Miamba ya soka la
Hispania vilabu vya Barcelona na Real Madrid vimendelea kutamba katika
ligi hiyo kwa kupata ushindi wa mabao mengi katika michezo yao.
Barcelona
waliichapa timu inayoburuza mkia katika ligi Osasuna, kwa mabao 7 -1
mabao ya Barca yakifungwa na Lionel Messi aliyefunga mabao mawili, Andre
Gomes, nae akafunga mawili kinda Francisco Alcacer, akatupia nae
magoli mawili huku Javier Mascherano, akifunga bao moja.
Leganes wakashinda kwa 3 - 0 dhidi ya Las Palmas, Nao Valencia wakalala nyumbani kwa kufungwa 3-2 na Real Sociedad.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni