Alhamisi, 18 Mei 2017

Baraza lapinga pendekezo la saa moja ya ngono Sweden

Per-Erik Muskos, diwani wa Övertorneå alipendekeza kuwapatia wafanyikazi hao mapumziko ya saa moja kila wiki

Per-Erik Muskos, diwani wa Övertorneå aliyependekeza kuwapatia wafanyikazi hao mapumziko ya saa moja kila wiki 
 
Madiwani katika baraza la mji mdogo wa Sweden wamepinga muswada wa pendekezo la kuwapa wafanyikazi wa manispaa, 'mapumziko ya kufanya tendo la ngono'
Per-Erik Muskos, diwani wa Övertorneå alipendekeza kuwapatia wafanyikazi hao mapumziko ya saa moja kila wiki kwenda nyumbani na kupata wakati bora wa kujamiana na wapenzi wao.
Aliiambia BBC kuwa lengo kuu lilikuwa kuimarisha uhusiano baina ya watu.
''Ni jina la herufi tatu{Sex} , ''Bw Muskos aliposema mwezi Februari, akipuuza wazo la kwamba anaingililia maisha ya watu binafsi.
Lakini wanachama wa baraza hilo ambao ni wahafidhina walipinga wazo hilo.
Meya wa Övertorneå, Tomas Vedestig, alihitimisha kwa kusema maisha ya kibinafsi ya wafanyakazi yanastahili kuwachwa vile yalivyo.
''Si kazi ya baraza kuingilia,'' aliambia SVT.
Bw Muskos alitumai kwamba kichwa cha mpango wa huo ungeongeza idadi ya watu katika mji wake ambao kwa hivi sasa idadi hiyo imezidi kushuka.
Mji wa Övertorneå kwa hivi sasa ni eneo ambalo lina watu 4,500 lakini wengi wao ni mwenye umri wa wastani.
''Vijana wengi huondoka mji huo pindi tu wanapokamilisha masomo yao, diwani huyo amesema.
Pia anadhani kwamba kutenga saa moja kwa wiki kutawasaidia wanandoa ambao hawana wakati na wapenzi wao.
''Watu wana vitu vingine vingi vya kufanya ,'' alisema. Ukiwa nyumbani watu wako kwenye mitandao, unahitajika kuwapeleka watoto kushiriki katika michezo ya soka na mpira wa magongo ya barafu, watu hawana muda .
Iwapo wafanyikazi wa 550 wa baraza wamekasirika, itakuwa nzuri  ya kutoa hasira katika hali hiyo mbaya: kwa sasa watumishi hao wana saa moja kwa wiki kushiriki katika michezo tofauti.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni