Alhamisi, 18 Mei 2017

NANI KASEMA ELIMU INA MWISHO: Waziri Mkuu wa zamani afaulu mtihani akiwa na miaka 82 India

Bw Chautala alihudumu kama waziri mkuu wa jimbo la Haryana kaskazini mwa India kwa mihula minne

 Bw Chautala alihudumu kama waziri mkuu wa jimbo la Haryana kaskazini mwa India kwa mihula minne
Waziri wa zamani ambaye anatumikia kifungo gerezaji baada ya kupatikana na kosa la kula rushwa amefaulu mtihani wa kumaliza shule India akiwa na miaka 82.
Om Prakash Chautala, aliyehudumu kama waziri mkuu wa jimbo la Haryana kaskazini mwa India kwa mihula minne, alifanya mtihani wa darasa la 12 akiwa katika jela ya Tihar mjini Delhi.
Mwanawe wa kiume Abhay Chautala alisema babake aliamua "kutumia vyema muda wake gerezani".
OP Chautala alipatikana na makosa kuhusiana na kuajiriwa kwa walimu.
Abhay Chautala aliambia gazeti la Indian Express kwamba babake amekuwa kila siku akienda kusoma katika maktaba ya gereza hilo.
"Husoma magazeti na vitabu. Huwa anawaomba wafanyakazi wa jela kumtafutia vitabu avipendavyo zaidi. Husoma vitabu kuhusu wanasiasa maarufu duniani, amesema.
Bw Chautala na 54 wengine, walipatikana na hatia ya kughushi vyeti walipokuwa wanawaajiri walimu 3,206 kati ya 1999 na 2000.
Waendeshaji mashtaka walisema watu waliokuwa wamehitimu zaidi walikataliwa na badala yake wale waliokuwa wametoa hongo wakaajiriwa.
Bw Chautala ni kiongozi wa chama cha Indian National Lok Dal Party na ni mwana wa aliyekuwa naibu waziri mkuu Devi Lal.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni