Jumatatu, 7 Agosti 2017

Kampuni ya bangi yaununua 'mji wa bangi' Marekani

Mikebe yenye bangi


Kampuni moja ambayo hutengeneza bidhaa za bangi imenunua mji mmoja katika jimbo la California kwa lengo la kuugeuza kuwa "kituo" cha bangi.
Kampuni hiyo ya American Green imekubali kuununua mji wa Nipton kwa $5m (£3.8m).
Kampuni hiyo itamiliki eka 120 za ardhi iliyojengwa mji huo, ambao unajumuisha shule, hoteli na duka moja kubwa.
American Green wanapanga kuzalisha nishati mbadala ambayo itakuwa ikitumiwa katika mji huo, bila kuchafua mazingira.
Mji wa Nipton, California unapatikana karibu na mpaka wa jimbo la Nevada.
"Tuna furaha isiyo na kifani kwamba sasa tunadhibiti eneo halisi la 'kijani'," rais wa American Green David Gwyther amesema kupitia taarifa kwa gazeti la Time.
"Mapinduzi ya bangi ambayo yanaendelea kwa sasa hapa Marekani yana nguvu za kubadili kabisa jamii sawa na jinsi dhahabu ilifanya katika karne ya 19."
  Marijuana edibles
Baadhi ya bidhaa zenye bangi
Mji wa Nipton ulianzishwa wakati wa pilika pilika za kutafuta dhahabu karne ya 20 dhahabu ilipokuwa inapatikana katika mgodi karibu na hapo.

Mji huo, ambao wakazi wake wa sasa ni 20 hivi, unapatikana katika mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Mojave.
American Green wanataka kuwekeza hadi $2.5m (£1.9m) kuufufua mji huo na kuufanya uvutie zaidi watalii na pia uwe wa kuzingatia mazingira

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni