Zaidi ya wanawake
50 katika majimbo yaliyo Kaskazini mwa India ya Haryana na Rajasthan
wamesema kuwa wamekatwa nywele zao wakati wakiwa hawana fahamu.
"Kulikuwa na mwanga mkali uliosababisha nipoteze fahamu. Saa moja baadaye niligundua kuwa nywele pia zilikuwa zimekatwa," alisema Sunita Devi, mwamamke mwenye umri wa miaka 53 kutoka Haryana.
"Nemeshindwa kulala wala kufanya chochote. Nilisoma kuhusu vituko hivi vikifanyika huko Rajasthan, lakini sikufikiria kingetendeka kwangu," aliongeza.
Mbali kidogo mwanamke mwingine Asha Devi naye alipoteza nywele zake katika shambulizi kama hilo siku iliyofuata.
Lakini wakati huo mshambuliaji aliripotiwa kuwa mwanamke.
Baba mkwe wake Asha Devi, Suraj Pal anasema kuwa kufuatia kisa hicho, alimshauri pamoja na wanawake wengine wa familia kuhamia nyumba ya jamaa wao kati jimbo la Uttar Pradesh.
Bwana Pal anasema alikuwa nyumbani wakati Asha Devi alitoka nje kufanya kazi zake.
"Nilienda nje kujua ni kwa nini hakurudi baada ya zaidi ya dakika 30. Tulipata amepoteza fahamu katika chumba cha kuoga. Nywele zake zilikuwa zimekatwa na kutupwa sakafuni."alisema.
Ripoti za kunyolewa wanawake kwanza ziliibuka mapema Julai kutoka jimbo la Rajasthan, lakini vituko sawa na hivyo kwa sasa vinaripotiwa kutoka Haryan na hata mji mkuu Delhi.
Sunita Devi anaishi katika jamii ya wafanya biashara na wakulima.
Baadhi wa majirani zake wanachukua zamu kukaa naye hadi apate kuondokewa na mshutuko.
Anasema mshambuliaji wake alikuwa ni mwanamume mzee ambaye alikuwa amevaa nguo nyeupe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni