Wanyama aina ya simba wakiwa katika hifadhi
Wakazi wa baadhi ya vijiji vinavyozunguka mbuga ya wanyama wa Kruger Nchini Afrika Kusini wanaishi kwa hofu baada ya simba wanne kutoroka katika mbuga hiyo na kuingia katika makazi ya watu.
Hali ilikuwa ya tafrani baada simba wanne kutoroka katika mbuga kubwa kabisa wanyama ya Kruger nchini Afrika. Madume manne ya simba yalitoroka Jumapili iliyopita kutoka katika mbuga hiyo, ambayo ni kivutio kikubwa kabisa cha utalii. Hali imekuwa ya wakazi kuchungulia milangoni kabla ya kutoka katika majumba yao kwa baadhi ya wakazi katika vijiji vilivyopo karibu na mbuga hiyo. Kataka taarifa yake ya awali mamlaka ya hifadhi ya mbuga za wanyama nchini Afrika Kusini, simba hao walionekana katika kijiji cha Matsulu. Maeneo yanayozunguka mbuga ya Kruger yanajumuisha vijiji kadhaa na mashamba ya mifugo, jambo ambalo kwa uhakika limewaweka watu wengi na mifugo yao katika hali ya wasiwasi wa kushambuliwa.Hili si tukio la mara ya kwanza kwani mwezi Mei mwaka huu, wahifadhi waliwatia mbaroni simba watano waliokuwa wametoroka. Mwaka 2015 simba maarufu katika mbuga nyingine tofauti na hiyo alipenya katika uzio wa umeme na kwa takribani wiki tatu akawa anaua ng'ombe kabla ya kukamatwa na askari wa wanyamapori.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni