Kampuni ya Apple imezindua simu mpya aina ya iPhone X ambayo hutumia utambulisho wa uso wako badala ya kidole kufunguka.
Apple
imesema kuwa simu hiyo inayojulikana kama Iphone 10 pia inaweza kutumia
utambulisho huo wa uso nyakati za usiku kufunguka na kwamba ni vigumu
kuidanganya ikilinganishwa na mfumo wa kutumia kidole.Ndio simu ghali zaidi kuzinduliwa na Apple.
Ikiwa na ukubwa wa kuhifadhi Gigabait 64 simu hiyo itagharimu £999 nchini Uingereza wakati itakapoanza kuuzwa rasmi mnamo mwezi Novemba tarehe 3.
Simu yenye ukubwa wa kuhifadhi Gigabait 256 itauzwa kwa £256 nchini Uingereza.
La kushangaza ni kwamba kampuni ya Samsung inauza simu yake ya aina ya Note 8 kwa £869 nchini Uingereza ikiwa na uwezo wa kuhifadhi Gigabait 64.
Kabla ya uzinduzi huo, Simu ya Apple iliokuwa ghali zaidi ni ile ya iPhone 7 Plus ambayo inagharimu $969 nchini Uingereza.
Mtaalam mmoja alisema kuwa uwezo wa Apple kuwashawishi wateja wake kugharamikia zaidi simu zake aina ya smartphone ni kitu cha heshima.
Simu hiyo inaweza kujichaji bila kutumia waya na haingii maji wala vumbi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni