Kijana wa miaka 17
kutoka nchini Canada ambaye alijitengenezea mwenyewe simu baada ya mama
yake Msomali kusema kuwa hana uwezo wa kumnunulia simu ya smartphone
amezungumza na BBC.
Mo Omer - ambaye anajiita "tech
nerd" - alitengeneza simu ya smartphone kuanzia mwanzo, na anasema
ataiuza kwa dola $180."Ina kila kitu unachoweza kukipata katika simu ya kawaida, ni kwamba tu haina gharama kubwa ," ameiambia BBC.
Simu "sio vifaa vigumu kutengeneza", aliongeza- na akasema ana azma ya kuzipeleka katika baadhi ya maeneo ya Afrika.
"Tumepokea maombi kutoka Nigeria na Algeria na maeneo mengine mengi. Ni soko linalokua kwa kasi ambalo tungependa kuingia "
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni