Jumamosi, 2 Septemba 2017

KENYATTA HOI RAILA KICHEKO baada ya Mahakama kufutilia mbali ushindi wa Kenyatta

  Rais uhuru Kenyatta akiwahutubia wafuasi wake jijini Nairobi. Alisema kuwa majaji waliobatilisha uchaguzi wkeni ni wakoraRais uhuru Kenyatta akiwahutubia wafuasi wake jijini Nairobi. Alisema kuwa majaji waliobatilisha uchaguzi wkeni ni wakora                


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amelitaja jopo la majaji wa mahakama ya juu liliobatilisha uchaguzi wake wa urais kuwa 'Wakora' .
Awali alikua ametaka kuwepo na utulivu na kusema kuwa ataheshimu uamuzi wa mahakama lakini baadaye akaonyesha msimamo tofauti katika mkutano wa hadhara.
Mahakama hiyo ilisema kuwa uchaguzi wa mwezi uliopita ulikumbwa na udanganyifu na kuagiza kufanyika kwa uchaguzi mwengine katika kipindi cha siku 60.
Uchaguzi huo uliokuwa umezua wasiwasi wa kutokea kwa ghasia za baada ya uchaguzi kama zile zilizotokea 2007.

Ijapokuwa ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi uliopita hazikufikia kiwango cha 2007, ghasia za siku kadhaa zilisababisha vifo vya watu 28.
Tume ya uchaguzi nchini Kenya ilikuwa imemtangaza rais Kenyatta kuwa mshindi kwa kiasi cha kura milioni 14 lakni matokeo hayo yakapigwa mahakamani na mpinzani wake mkuu Raila Odinga.
Katika uamuzi wake Jaji mkuu David Maraga alisema kuwa uchaguzi huo wa tarehe 8 mwezi wa nane haukufanyika kulingana na katiba na hivyo basi kubatilisha matokeo yake.
Katika hotuba aliyotoa katika runinga, rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa ni muhimu kuheshimu sheria hata iwapo unatofautiana na uamuzi wa mahakama ya juu.
Alitaka kuwepo kwa utulivu akisema: Jirani yako ataendelea kuwa jirani yako licha ya lololote litakalotokea.
Ujumbe wangu muhimu leo ni Amani. Lakini alikuwa na msimamo mwingine wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika soko moja jijini Nairobi.
Raila Odinga akifurahia uamuzi wa mahakama uliofutilia mbali uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta                                   Raila Odinga akifurahia uamuzi wa mahakama uliofutilia mbali uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta                
Aliwataja jaji Maraga na majaji wenzake kuwa ni wakora, akisema aliamua kubatilisha uchaguzi wake.
Alimuonya jaji Maraga kwamba baada ya uchaguzi huo kufutiliwa mbali bado yeye ndio rais na sio tena rais mteule kama ilivyokuwa.
Mnanielewa? Maraga anafaa kujua kwamba hivi sasa anakabiliana na rais aliye madarakani, alisema bwana Kenyatta mwenye umri wa miaka 55.
Tunawaangalia kwa karibu. Lakini wacha tumalize uchaguzi mwanzo, Hatuogopi.
Kufuatia uchaguzi huo waangalizi wa kimataifa kutoka muungano wa Ulaya, ule wa Afrika pamoja na wale wa Marekani walikuwa walisema kuwa hakuna udanganyifu uliofanyika na kumtaka Odinga kukubali kushindwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni