Polisi nchini Argentina walimpiga risasi njiwa ambaye alitumiwa kusafirisha mihadarati kwenda gereza moja, kwa mujibu wa mamlaka za gereza.
Njiwa huyo alionekana akiruka hadi uwanja wa gereza lililo mji wa Santa Rosa.
Maafisa waligundua kuwa ndege huyo alikuwa amefungiwa mfuko mdogo kwenye mgongo wake uliokuwa na tembe za madawa ya kulevya.
Njia hiyo ya kusafirisha madawa ilikuwa imegunduliwa na ilikuwa ikifanyiwa uchunguzi.
Gazeti la Clarin lilichapisha picha ya njiwa huyo akiwa na mfuko mweupe uliokuwa na tembe 44 za madawa ya kulevya.
Magereza nchini Argentina yalionya mwaka 2013 kuwa walanguzi wa madawa ya kulevya walikuwa wakitumia njiwa waliokuwa wakifanya safari mara 10 hadi 15 kwa siku.
Watu watatu walikamatwa na njiwa 15 kupatwa baada ya uchunguzi wa mwaka 2013.
Mapema mwaka huu njiwa ambaye alikuwa na mfuko uliokuwa na tembe 178 za dawa ya kulevya alishikwa nchini Kuwait karibu na mpaka na Iraq.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni