Spika
Ndugai leo amewausia wabunge wanzake kuwa makini na usalama wao kwa
kuchukua hatua zaidi za kujilinda, ikiwemo kutokaa baa mpaka usiku wa
manane ili kujiepusha na matatizo mbali mbali yatakayoathiri usalama
wao. .
Akizungumza muda mfupi leo Ijumaa kabla ya kuahirishwa kwa Bunge, Ndugai aliwataka wabunge kutokaa sana katika mabaa.
“Yaani
tuchukue hatua katika maisha yetu kama mnavyosikia matukio ni mengi
katika nchi yetu. Ni vizuri usalama unaanza na wewe mwenyewe
kwanza,” amesema.
Amesema vyombo vya usalama vinavyowalinda vinakuwa vinaongezea kidogo na kuwataka kutazama nyendo zao za namna ambavyo wanaishi.
“Kwa
wale tuliozoea saa 7 ndio tunarudi nyumbani basi tuanze kurudi
mapema kidogo. Lakini pia tuangalie usalama wa familia zetu na tuwaambie
wapigakura naona siku hizi watoto wanapotea, watoto wanauawa,” amesema.
Amewataka
wabunge kuwapelekea familia ujumbe huo kuwa wawe makini na watoto wao wakati wa
kwenda shule na maeneo mengine kwa kuhakikisha wanajua mtu
anayewapeleka shule na kuwachukua.
“Hayo mambo yanayofanana na hayo. Ushauri ni wa ujumla tu,”amesema.
Aliwataka wabunge kuendelea kumuombea Tundu Lissu na wale watakaopata nafasi ya kwenda kumuona jijini Nairobi wampelekee ujumbe.
Amesema pia wabunge wawaombee wenzao ambao wamekwenda kumuuguza mbunge huyo lakini wanatukana kwa sababu hawajui watendalo.
Ushauri huo umekuja siku chache baada ya Lissu kujeruhiwa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni