Mkazi mmoja wa mji
wa Oslo anajutia aliyoyafanya akiwa amelewa mkesha wa Mwaka Mpya baada
ya kugundua kwamba alikuwa anadaiwa $2,220 (£1,640) sawa na shilingi za Kitanzania milioni 5 kwa kutumia teksi.
Mwanamume
huyo wa miaka 40 hivi alikuwa amesafiri kupitia mataifa matatu, kuanzia
Copenhagen nchini Denmark, akapitia Sweden, na kisha akafika Oslo
nchini Norway.Alipofika nyumbani, aliingia ndani na hakumlipa nauli dereva wa teksi.
Dereva huyo alijipata amekwama baada ya betri ya gari lake yake kuisha chaji akiwa nje ya nyumba ya mwanamume huyo akisubiri atoke nje na pesa amlipe.
Aliamua kuwapigia simu polisi.
Kupitia Twitter, polisi wa Olso wanasema walimkuta mwanamume huyo akiwa amelala fo fo fo kitandani na kumwamsha.
Alikubali kulipa pesa alizokuwa anadaiwa.
Mwanamume huyo hana historia ya kutekeleza uhalifu, kwa mujibu wa runinga ya taifa ya Norway ya NRK.
Safari hiyo ya kutoka Copenhagen hadi mtaa wa Abildso mjini Oslo ilikuwa ya umbali wa 600 km (maili 372).
Huenda akafikiria kutumia ndege siku zijazo...
Na dereva wa teksi? Gari jingine lilifika kumsaidia..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni