Jumatano, 18 Aprili 2018

Nape Nnauye Ahoji Kuhusu Soko la Mbaazi Bungeni.......Serikali Yajibu Soko ni Baya, Watanzania Waitumie Kula Maana ni Chakula Kizuri


SeeBait
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameuliza serikali imefikia wapi kutafuta soko la Mbaazi baada ya msimu uliopita matatizo ya soko kushusha bei kutoka Tshs 2,000 mpaka 150. Amesema serikali iliahidi Bungeni kuwa itahakikisha inahangaika kupata soko la kuaminika la zao hilo.

Nape amesema sasa ni msimu wa kilimo hicho, kama bado hali haieleweki wananchi washauriwe waachane na mbaazi na badala yake wajikite kwenye mazao mengine ambayo yana soko la uhakika.

Akijibu swali hilo naibu waziri wa kilimo, Eng. Stella Manyanya amemjibu kuwa ni kweli hakukuwa na hali inayoridhisha kwenye soko la mbaazi na ni kutokana na wadau waliokuwa wanategemewa sana ilikuwa ni India.

Neema yaja kwa watumishi wa umma


SeeBait
SERIKALI imetangaza neema kwa watumishi wa umma 4,812 baada ya jana kubainisha kuwa kuna fursa za mafunzo 659 zitakazotolewa na Serikali ya China.

Fursa hizo za mafunzo zimejikita kwenye maeneo ya kipaumbele cha taifa yaliyoainishwa katika Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21).

Katika mkutano wake na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari na Elimu ya Bunge mjini hapa jana, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema mafunzo yamejikita kwenye uhandisi wa viwanda, mawasiliano na usafirishaji.

Dk. Ndumbaro pia alisema mafunzo hayo yatajikita kwenye kilimo, elimu, afya, biashara na uchumi, Tehama na utawala bora.

Serikali Kuajiri Walimu 6,000 June


SeeBait
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imesema hadi kufikia Juni 30 mwaka huu inatarajia kuajiri walimu 6,000 wa masomo ya Hisabati na Sayansi kwa ajili ya shule za sekondari nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Joseph Kakunda, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali, ambaye alitaka kujua mikakati ya serikali katika kuondoa changamoto katika shule za kata ikiwamo upunguzu wa walimu wa Hisabati na Sayansi.

Pia, Bobali alitaka kujua msimamo wa serikali kuhusu wananchi kuchangia kwenye chakula ambacho wameona ndio chachu ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi katika Mkoa wa Lindi. Alisema hadi Desemba mwaka 2017, Serikali ilikuwa imeajiri walimu 200 wa Hisabati na Sayansi kwa ajili ya shule za sekondari.

Kadhalika, alisema serikali haijazuia wananchi kuchangia maendeleo ya shule walichokataza ni kumzuia kumpa adha ya kukosa masomo mwanafunzi ambaye ameshindwa kuchangia michango hiyo.

AJIRA ZA UTUMISHI WA UMMA 2017- 2018

Cheki www.mabumbe.com