Ijumaa, 9 Mei 2014

MENO YA TEMBO YAIBWA KITUO CHA POLISI

Polisi akilinda sehemu ya shehena ya meno ya tembo iliyokamatwa Dar es Salaam hivi karibuni. Picha ya Maktaba
Meno ya tembo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya vielelezo mahakamani yalitoweka katika Kituo cha Polisi cha Kilwa mkoani Lindi. Tukio hilo limenukuliwa katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ikisema meno makubwa 108 ya tembo na kilo 20 za meno mengine ya tembo yaliyokuwa yamehifadhiwa kama kielelezo cha kesi za uhujumu uchumi, yamebainika kutoweka kinyemela. Ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni juzi, imebainisha kuwa meno mengine makubwa ya tembo yaliyokuwa na uzito wa kilo 498.3 yamebadilishwa kinyemela na meno madogo, hivyo kusababisha hasara ya kilo 203.66 za meno ya tembo ambazo thamani yake haikufahamika.CAG Ludovick Utouh katika ripoti hiyo ya mwaka ulioishia Juni 30, 2013, amebainisha kuwa kumbukumbu katika Pori Tengefu la Miguruwe zilionyesha kuwa katika kipindi cha kuanzia Juni 5 hadi Juni 8, 2012 meno makubwa 108 yalikuwa miongoni mwa vielelezo kituoni hapo.Kati ya meno hayo 108 yaliyokamatwa katika matukio ya ujangili, 74 yalitoweka katika kituo cha polisi wakati 34 yalibadilishwa na meno madogo, tofauti na yale yaliyokuwa yamekamatwa yakihusishwa na kesi ya ujangili Na. 3/2009 na kesi nyingine ya uhujumu uchumi Na. 2/2010 ambazo zilikuwa zikiendelea mahakamani mkoani Lindi.
Pia ilibainika kuwa kilo 20 za meno ya tembo ambayo yalikamatwa na kuhifadhiwa kama kielelezo cha majalada KLM/IR/184/2009, KLM/IR/235/2009 na KLM/IR/567/2010 yalitoweka.
Gari la ujangili latowekaUkaguzi huo pia ulibaini kuwa gari lililokamatwa likiwa kielelezo baada ya kukutwa na kilo 26 za meno ya tembo yenye thamani ya Sh135 milioni liliondolewa kinyemela katika Kituo cha Polisi Kilwa.CAG katika ukaguzi huo alibaini upungufu katika usimamizi wa meno ya tembo na nyara nyingine za taifa katika chumba cha meno hayo Dar es Salaam na vituo vya mikoani.CAG katika taarifa yake hiyo amesema kutokana na kukosekana kwa kumbukumbu sahihi, meno ya tembo yanaweza kuibwa au kupotea bila menejimenti kuwa na taarifa yoyote, hivyo ameishauri Serikali kuhakikisha kunakuwa na udhibiti wa kutosha katika usimamizi wa nyara za Serikali nchi nzima.
MWANANCHI

NJEMBA YANASWA NA MADINI FEKI


Kijana aliyefahamika kwa jina la Samson Ntemi aliyetuhumiwa kwa utapeli wa madini bandia
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Samson Ntemi (44) mkazi wa Msingwi, Wilaya ya Magu mkoani Mwanza amenaswa na Polisi wakati akifanya jaribio la utapeli wa madini feki huko Kijitonyama jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kwa mujibu wa chanzo makini, mtu huyo alianza harakati za utapeli wake kwa kumpigia simu mfanyabiashara mmoja wa magari akimweleza kuhusu nia yake ya kununua gari aina ya Canter kutoka kwake kwa kiasi cha shilingi milioni 32.
Chanzo kilisema kufuatia simu mfululizo za mtu huyo, mfanyabiashara huyo alipata hofu na kuhisi huenda alikuwa ni tapeli, hivyo kuweka mtego na kumtaka wakutane Mwananyamala kwa ajili ya kufanya biashara hiyo. Lakini hata hivyo, walipokutana tapeli huyo alimtaka mfanyabiashara huyo kuongozana naye hadi Kurasini, akidai ndipo alipokuwa mteja mwenye kulihitaji gari hilo.
“Nilishangaa jamaa akinibadilishia kauli akidai anayetaka gari ni bosi wake siyo yeye.
Nilipomhoji vizuri akaniambia yeye ni mfanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Ifakara, mkoani Morogoro aliyefika Dar kutafuta soko huku akionesha kutolijua vizuri Jiji la Dar”. Chanzo chetu kilimnukuu mfanyabiashara huyo akisema.
Inadaiwa kuwa tapeli huyo alimwonyesha mfanyabiashara huyo madini hayo yenye thamani ya mamilioni ya shilingi na kumtaka anunue. Baada ya kuyaona na kugundua kuwa ni feki, alimtaka tapeli huyo kuandamana naye hadi benki maeneo ya Kijitonyama ili amkabidhi fedha.
Wakiwa njiani, mfanyabiashara huyo aliwasiliana na Polisi wa Kituo Kidogo cha Mabatini, Kijitonyama ambao walikuja eneo la tukio na kumkamata tapeli huyo, aliyekiri mbele ya askari kuwa alishawahi kufanya wizi huo katika miji ya Tarime, Arusha na Shinyanga. (TK)

Alhamisi, 8 Mei 2014

"MVUA YA SAMAKI" YANYESHA NCHINI SRI-LANKA


Samaki waliotoka mtoni kutokana na upepo mkali

Wakazi wa kijiji kimoja Magharibi mwa Sri Lanka wamesema kuwa wameshangazwa na pia kufurahishwa na tukio la 'kunyeshewa' na mvua ya Samaki wadogo.

Samaki hawa ambao walikuwa katika hali nzuri ya kuweza kulika wanaaminika kuwa walibebwa kutoka kwa mto kwa upepo mkali.

 

Wanakijiji hao wa wilaya ya Chilaw walisema kuwa walisikia kitu kizito kikianguka na wakapata samaki wengi wenye uzani wa kilo hamsini .

Hili si tukio la kwanza la aina hii kuwahi kutokea Sri Lanka- mwaka wa 2012, kulitokea kisa cha mvua ya viumbe vya baharini vijulikanavyo kama 'Kamba' ambavyo huliwa

Wanasayansi wamesema kuwa mvua ya Samaki hutokea wakati ambapo upepo mkali unazinga juu ya maji ya kina kifupi na hivyo kusababisha mzunguko wa maji unaovuta karibu kila kitu kilicho ndani ya maji ikiwa ni pamoja na samaki na hata Vyura.

Wakazi wanasema sio mara ya kwanza kwa mvua ya Samaki kuwanyeshea

Viumbe hawa wa majini wanaweza wakasafirishwa kwa masafa marefu kwa kushikiliwa na mawingu hata baada ya ule mzunguko wa maji kuisha.

Wanakijiji wanasema kuwa mvua hiyo ya Samaki ilinyesha Jumatatu huku viumbe wale wakianguka kwenye mashamba, barabara na paa za kijiji hicho.

Baadhi ya samaki hao wenye urefu wa kati ya sentimita tano na nane, walikuwa bado wako hai na walitiwa kwenye ndoo za maji na wanakijiji waliowatumia kama kitoweo baadaye.

Hii ni mara ya tatu kwa tukio kama hili kufanyika Sri Lanka, ingawa katika eneo tofauti.

Kando na ile mvua ya ‘Prawn’ya mwaka wa 2012 kusini mwa Sri Lanka, mvua ya kimondo (meteors) nyekundu na manjano ilinyesha mwaka huo huo, tukio ambalo bado linachunguzwa na wanasayansi wa Marekani na Uingereza.

Samaki wana dhamana kuu Sri Lanka

SERIKALI KUFUNGAMFUMO MAALUM WA KUJAZA MAFUTA KWENYE MAGARI NA MITAMBO TAASISI ZA UMMA

1 (1)Mkurugenzi wa Ununuzi na Ushauri toka wakala wa huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) bw. Yoswam Nyongera akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uwezo wa mfumo wa kielektroniki utakaotumika kujaza mafuta katika magari na mitambo ya Serikali ikiwemo kutunza kumbukumbu za malipo ya mafuta na hivyo kutoa mafuta kwa kadiri ya fedha iliyolipwa na Taasisi husika.
2 (1)Mkurugenzi wa Uendeshaji toka wakala wa huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) bw. Naftal Singwejo akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu mfumo mpya wa kielektroniki utakaotumika katika kutoa huduma ya mafuta kwa magari ya Serikali na mitambo ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma hiyo kwa Taasisi ,Wakala na Wizara zote .kushoto ni Mkurugenzi Himili Biashara Bw. Malik Aram. Frank Mvungi-Maelezo
Serikali yaanza kutekeleza mradi wa kufunga mfumo wa kielektroniki kujaza mafuta magari na mitambo ya taasisi za Umma ili kuongeza tija katika utoaji huduma hiyo kote nchini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) bw. Naftal Singwejo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua Singwejo amesema mradi huo utashirikisha Wizara,Taasisi zote za Umma,Wakala na Idara zinazojitegemea ambazo kwa mujibu wa sheria ya ununuzi wa Umma na 7 ya Mwaka 2011 sura ya 410 kifungu cha 56 zinatumia huduma hiyo toka kwa wakala huo.
“Hatua za awali za utekelezaji wa mradi huu zitahusisha kufungwa kifaa maalum (identification tag) katika mlango wa tanki la gari au mtambo “alisema Singwejo
Akizungumzia faida za mfumo huo, Singwejo alisema hakutakuwa na mfanyakazi (Pump Attendant) wa kuweka mafuta katika gari au mtambo na hivyo huduma hiyo itapatikana kwa haraka na hivyo kuongeza tija.
Faida nyingine ni kuwa taarifa ya matumizi ya mafuta ya chombo cha umma itapatikana kwa wakati kwa njia ya mtandao na hivyo maamuzi sahihi kufanyika juu ya matumizi ya mafuta kwa chombo husika.
Aidha, Singwejo alibainisha kuwa mfumo huo utaondoa kabisa udanganyifu wa matumizi ya mafuta katika magari na mitambo kwa taasisi za umma na kutoa nafasi kwa chombo kilichodhibitika tu kuweza kupata huduma ya mafuta.
Naye Mkurugenzi Himili Biashara Bw. Malik Aram alisema kuwa mfumo huo ni wa kisasa ambao unatumika katika nchi zilizoendelea na majaribio ya mfumo huo hapa Tanzania yatafanyika katika kituo cha Kurasini mwishoni mwa mwezi Julai, 2014 ambapo hadi sasa mfumo huo umeanza kusimikwa katika kituo hicho.
Bw. Malik aliongeza kuwa baada ya kukamilika kwa mfumo huu katika kituo cha Mafuta cha kurasini katika mwaka huu wa fedha katika mwaka ujao wa fedha mfumo huo utafungwa katika Mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Mbeya, na Mwanza.
Serikali ilianzisha wakala wa Huduma ya ununuzi Serikalini (GPSA) ili kudhibiti matumizi ya fedha za umma yanayofanyika kupitia ununuzi wa vifaa mbalimbali na mafuta kwa ajili ya magari na mitambo ya umma, hivyo mfumo huu ni moja ya hatua za utekelezaji wa mpango huo kamambe wa kuwa na matumizi ya rasilimali za umma wenye tija

BOKO HARAMWAKIRI KUTEKA WASICHANA ZAIDI YA 200 NIGERIA


Wasichana waliotoroka mikononi mwa Boko Haram

Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau.

Kundi la kislamu nchini Nigeria la Boko Haram linasema kuwa ndilo lililowateka nyara zaidi ya wasichana wa shule 200 ambao hawajulikani waliko kwa wiki tatu sasa.

Kupitia kwa njia ya video kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau amesema kuwa watawauza wasichana hao. Wasichana hao walitekwa kutoka shule moja iliyo kaskazini mashariki mwa nchi.

ALAZWA HOSPITALI KWA MIAKA 45


Lanjui aliyelazwa katika Wodi Namba Nne katika hospitali hiyo tangu Januari Mosi, 1971, awali alilazwa katika Hospitali ya Sekou Toure, Mwanza kuanzia mwaka 1969 mara baada ya kupata ajali.

SINGIDA.

Usiombe yakupate. Abdi Lanjui (75), ametimiza mwaka wa 45 akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa wa Singida alikolazwa tangu mwaka 1971 baada ya kupata ajali ya lori.
Lanjui aliyekuwa dereva wa taasisi aliyoiita “Mamlaka ya Pamba,” alipata ajali hiyo mkoani Mwanza baada ya lori alilokuwa akiendesha kuchomoka gurudumu la mbele na kupinduka.


“Sababu ya mimi kugeuza wodi kuwa makazi yangu ya kudumu ni ajali iliyosababisha kupooza kuanzia kiunoni hadi kwenye nyayo. Kwa kuwa sinyanyuki kitandani, nimepata vidonda kuanzia makalioni hadi miguuni. Kwa sasa naishi maisha magumu mno,” alisema.


Aomba msaada
Kutokana na hali hiyo, ameiomba Serikali na jamii kwa jumla kumsaidia chakula kwa kuwa hana ndugu wa kumsaidia. Lanjui ambaye hawezi kunyanyuka kitandani, alisema kwa miaka mingi uongozi wa hospitali ya mkoa ulikuwa ukimhudumia kwa kumpa chakula lakini baadaye huduma hiyo ilisitishwa, hivyo kumfanya awe ombaomba na maisha yake kuwa ya mlo mmoja kwa siku.


“Kwa vile siwezi kunyanyuka kitandani na sina ndugu yeyote, nimekuwa nikiwaomba msaada manesi na watumishi wengine wa hapa hospitali. Nashukuru sana wamekuwa wakinisaidia bila kuchoka na kuniwezesha kupata walau mlo wa siku moja,” alisema. Lanjui ambaye anazungumza vizuri pia aliomba msaada wa fedha za kwenda Hospitali ya KCMC, Moshi ili apatiwe huduma zaidi ya matibabu.


Mwanza hadi Singida
Lanjui aliyelazwa katika Wodi Namba Nne katika hospitali hiyo tangu Januari Mosi, 1971, awali alilazwa katika Hospitali ya Sekou Toure, Mwanza kuanzia mwaka 1969 mara baada ya kupata ajali.


Alisema akiwa Sekou Toure mwishoni mwa mwaka 1970, hali yake ilibadilika na kuwa mbaya ndipo alipomwomba mwajiri wake amrudishe nyumbani katika Kijiji cha Mhintiri katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ili ‘akasubiri kifo chake.’


Hata hivyo, alisema uongozi wa Mamlaka ya Pamba ulikataa kumpeleka kijijini kwake, badala yake ulimkabidhi katika Hospitali ya Mkoa wa Singida mwaka 1971.


Alisema wakati anapata ajali na kulazwa hospitalini, wazazi na ndugu yake wa pekee, walikuwa wamekwishafariki dunia.


Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Mussa Kamala alisema hivi sasa mgonjwa huyo anahudumiwa na hospitali kama watu wengine wenye ulemavu ambao hawatozwi gharama yoyote.MWANANCHI

MAN CITY WAKARIBIA UBINGWA EPL

 
Man of the hour: Edin Dzeko roars to the Etihad stands after his first goal gives City the lead
Mtu wa heshima: Edin Dzeko akiunguruma baada ya kufunga bao lake la kwanza leo Etihad dhidi ya Aston Villa.
KWA asilimia kubwa mnuso wa ubingwa wanukia Etihad baada ya Manchester City kuibuka na ushindi mtamu wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England.
Ushindi huu umewarejesha Man City kileleni na sasa wanahitaji pointi moja tu kutwaa taji msimu huu.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa milango ya timu zote kuwa migumu.

Jumatatu, 5 Mei 2014

WAHABESHI 55 WANASWA HIMO MOSHI


Waethiopia 55 wamekamatwa na wanakijiji cha Chekereni Pabliki kilichopo Himo, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakiwa wamejificha kichakani na mkazi mmoja wa kijiji hicho.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, amethibitisha kutokea tukio hilo na kwamba watu hao walikamatwa
“Wanakijiji walitoa taarifa polisi baada ya kuwaona watu hao, na sisi tulifika mara moja kuwakamata wakiwa na mwenyeji wao,” alisema Kamanda Boaz.
Aliongeza: “Kwa sasa hatuwezi kumtaja jina wenyeji wa watu hao kwa vile bado tunaendelea na uchunguzi zaidi.”
Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, watu hao baada ya kuhojiwa walidai kuwa walikuwa njiani kwenda nchini Afrika Kusini kupitia Tanzania.
Alisema uchunguzi unaendelea ili kubaini wahusika wengine zaidi wa mtandao wa kusafirisha binadamu kabla ya kufikishwa mahakamani.
Aliwataka wananchi waishio mipakani kuendelea kuwa walinzi na kutoa taarifa polisi pindi wanapowaona watu wanaowatilia shaka katika maeneo yao.

MSIMAMO WA LIGI KUU YA UINGEREZA


#
Team
GP
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
36
25
5
6
96
37
59
80
2
36
25
5
6
96
46
50
80
3
37
24
7
6
69
26
43
79
4
37
23
7
7
66
41
25
76
5
37
20
9
8
59
39
20
69
6
37
20
6
11
52
51
1
66
7
36
18
6
12
60
41
19
60
8
37
15
10
12
53
45
8
55
9
37
15
4
18
42
57
-15
49
10
37
12
11
14
43
51
-8
47
11
36
13
4
19
28
43
-15
43
12
37
11
7
19
40
49
-9
40
13
37
10
9
18
51
53
-2
39
14
36
10
8
18
39
54
-15
38
15
36
10
7
19
37
48
-11
37
16
36
7
15
14
42
55
-13
36
17
36
9
8
19
38
57
-19
35
18
37
8
9
20
28
60
-32
33
19
37
9
4
24
38
83
-45
31
20
37
7
9
21
31
72
-41
30

Ijumaa, 2 Mei 2014

POLISI MACHINGA WACHAPANA KARIAKOO

Jeshi la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) katika Soko Kuu la Kariakoo.
Hamisha hamisha hiyo yenye baraka za uongozi wa mkoa zilianza mapema mwezi uliopita kwa lengo la kuondoa biashara zisizo rasmi katikati ya jiji la Dar es Salaam, pamoja na bodaboda, bidhaa zimwagwazo chini, mama ntilie na vibanda vya vocha.
Majira ya saa tisa alasiri magari ya polisi yaliwasili sokoni hapo huku yakiwa na askari polisi na mgambo waliokuwa wamevaa fulana na kofia za Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), zenye rangi ya njano, na kuanza kuwakamata wamachinga hao.
Askari hao waliokuwa katika magari aina ya Land Rover Defender na Toyota LandCruiser waliuvamia mitaa ya Kongo na Mchikichini kufanya oparesheni hiyo kabla hawajalazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwaondoa walengwa katika eneo hilo.