Jumapili, 1 Machi 2015
Jumamosi, 28 Februari 2015
CC YAWASIMAMISHA TIBAIJUKA, CHENGE NA NGELEJA
KAMATI KUU ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo
tarehe 28/8/2015, kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi na moja alasiri,
kimeazimia yafuatayo;Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, msanii wa Chama na Kada wa muda
mrefu Mheshimiwa John Damian Komba.
Mwenyekiti wa CCM, Mhe Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea
kuwa msiba huo ni pigo kubwa kwa Chama hasa katika wakati huu wa kuelekea kwenye
uchaguzi na pengo ambalo ni vigumu kuliziba.
CCM imepata pigo na Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti inatoa
pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Kapteni John Damian Komba.
Kazi yake kubwa ndani ya Chama itaandikwa katika historia
iliyotukuka ya Chama Cha Mapinduzi.
> Pia, kutokana na Kikao cha Kamati Kuu iliyopita
iliyoiagiza kamati ya maadili kuwaita na kuwahoji wanachama na viongozi watatu
waliotajwa kuhusika na kashfa ya Escrow ambao ni Mheshimiwa Anna Kajumulo Tibaijuka, Mheshimiwa William Mganga Ngeleja na Mheshimiwa Andrew Chenge.
Baada ya Kamati ya Maadili kuwahoji, Kamati Kuu imeazimia
kuwasimamisha kuhudhuria vikao ambavyo wao ni wajumbe ikiwemo Kamati kuu kwa
Mama Tibaijuka na Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Mheshimiwa Chenge na
Ngeleja.,wakati ambapo kamati ndogo ya maadili ikiendelea na uchunguzi wa
kuhusika kwao katika kashfa hiyo.
> Pia, Kamati Kuu imejadili suala la Adhabu iliyotolewa
kwa wanachama sita ambao walibainika kuvunja Kanuni na sheria za Chama kwa
kuanza Kampeni kabla ya wakati na imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuendelea
kuchunguza mienendo ya wanachama hao katika kipindi walichokuwa wanatumikia
adhabu zao. Na kisha taarifa hiyo ya Kamati ndogo ya maadili itawasilishwa kwa
Kamati Kuu.
AZAM NJE LIGI YA MABINGWA YACHEZEA KICHAPO CHA 3-0
AZAM YANG’OLEWA CAF, YACHAPWA 3-0
Azam FC imeng’oka katika michuano ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika
baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa El Merreikh.
Azam FC ilishinda kwa mabao 2-0 jijini Dar, hivyo kufanya ing’oke kwa jumla ya mabao 3-2.
Katika mechi iliyochezwa leo jijini Khartoum, Sudan, Azam FC ilianza kukubali bao katika dakika ya 11 mfungaji akiwa Coffie.
Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza na ilikuwa ni kuhakikisha Azam wanakomaa hadi mwisho, lakini ikashindikana.
Merreikh ilipata mkwaju wa penalti kutokana na faulo ya Serge Wawa, lakini ikakosa.
MCHINJAJI WA IS NI MWINGEREZA
Mwanamgambo anayejulikana kwa jina la utani 'Jihadi John' wa kundi la
wanamgambo wenye itikadi kali la dola la kiislamu IS, ambaye amekuwa
akionekana katika video akiwachinja mateka ametambuliwa kama Mohammed
Emwazi
Mohammed Emwazi ni raia wa Uingereza, mtaalamu wa masuala ya programu za
kompyuta anayetokea familia inayojiweza iliyoko mjini London na alikuwa
akifahamika na maafisa wa usalama nchini Uingereza hata kabla ya
kuelekea Syria.Mwanamgambo huyo ambaye huonekana katika video za kundi la IS akiwa amevalia nguo nyeusi na kuufunika uso wake, kushikilia kisu na kuzungumza kizunguchenye lafudhi ya Kiingereza anaaminika kuwa mchinjaji wa mateka wa kundi hilo wakiwemo raia wa Marekani, Uingereza na Syria.
MAN U YAUNGURUMA
Mkwaju
wa penalti uliofungwa na nahodha Wayne Rooney uliisaidia Manchester
United kuichapa Sunderland mabao 2-0 baada ya West Brown kupewa kadi
nyekundu katika kile kilichoonekana kama maonevu.
Rooney alifunga
baada ya mshambuliaji Radamel Falcao kuchezewa visivyo na kusababisha
kutolewa kwa Wes Brown badala ya John Oshea aliyecheza vibaya licha ya
pingamizi kutoka kwa mashabiki.Manchester united iliongeza bao la pili baada ya Rooney kufunga kupitia kichwa baada ya mkwaju wa Adnan Januzaj kupanguliwa na kipa.
Ushindi huo umeimarisha harakati za kilabu hiyo kuwania nafasi nne bora katika ligi hiyo.
Matokeo mengine:
West Ham 1 - 3 Crystal Palace
Burnley 0 - 1 swansea
Newcastle 1 - 0 Aston Villa
Stoke 1 - 0 Hull
West Brom 1 - 0 Southampton
MWANASIASA MAARUFU AUAWA NCHINI URUSI
Boris Nemtsov kiongozi wa upinzani mwenye heba na mkosoaji mkubwa wa
rais Vladimir Putin wa Urusi ameuawa kwa kupigwa risasi karibu na Ikulu
Moscow Ijumaa usiku. (27.02.2015).
Kifo chake kinakuja siku moja kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanyika
dhidi ya serikali hapo Jumapili ambapo alikuwa akitazamiwa kuhudhuria.Kifo cha Nemtsov, mwenye umri wa miaka 55 naibu waziri mkuu wa zamani, kimezusha hasira miongoni mwa viongozi wa upinzani ambao wameishutumu serikali ya Urusi kwa kujenga hali ya kutovumilia upinzani wowote na kuyaita mauaji hayo ni ya kukusudia.
Rais Putin haraka alituma salamu zake za rambi rambi na kuyaita mauaji hayo kuwa ni ya uchokozi.
MHE WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI NYUMBA ZA WATUMISHI MBEYA
Waziri
Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda akifungua kitambaa kuashiria kuweka
jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo.
Waziri
Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda, akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa
Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio wakati akiwasili katika eneo
la mradi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya
Wialaya ya Busokelo, Mbeya.
Waziri
Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda, akisalimiana na Meneja Miradi wa
NHC, George Magembe wakati akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za
gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wialaya ya Busokelo,
Mbeya.
Baadhi
ya watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Wakiongozwa na Kaimu
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio wakipokea
wageni waliokuwa wakiwasili katika eneo la nyumba za gharama nafuu za
watumishi za Busokelo, Mbeya zinazojengwa na Shirika hilo na kuwekwa
jiwe la msingi na Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Mojawapo ya nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Busokelo zinazojengwa na NHC kama zinavyoonekana leo.
Msoma Hotuba wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Bw. Sanga akisoma hotuba hiyo mbele ya Waziri Mkuu leo.
Waziri
Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda, akijadiliana jambo na Kaimu
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) na Mbunge wa Rungwe Mashariki ,
Profesa Mark Mwandosya katika eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu
za watumishi wa Halmashauri ya Wialaya ya Busokelo.
Waziri
Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda, akijadiliana jambo na Kaimu
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) na Mbunge wa Rungwe Mashariki ,
Profesa Mark Mwandosya katika eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu
za watumishi wa Halmashauri ya Wialaya ya Busokelo.
Baadhi ya Watendaji wa NHC na viongozi wa Wilaya ya Busokelo mkoani Mbeya wakiwa wamejipanga kumkaribisha Waziri Mkuu
Waziri
Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda akikaribishwa na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais (Kazi Maalumu) na Mbunge wa Rungwe Mashariki , Profesa Mark
Mwandosya wakati akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za gharama
nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Mbeya.
Kaimu
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio akizungumza na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) na Mbunge wa Rungwe
Mashariki , Profesa Mark Mwandosya katika eneo la nyumba za gharama
nafuu za watumishi za Busokelo, Mbeya zinazojengwa na Shirika hilo kabla
ya kuwekwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Baadhi ya Wafanyakazi wa NHC wakifuatilia uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi huo wa nyumba za watumishi wilayani Busokelo. MHE WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI NYUMBA MBEYA
Waziri
Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda akifungua kitambaa kuashiria kuweka
jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo.
BREAKIN NEWZZZZ: MHE JOHN KOMBA AMETUTOKA
Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba amefariki Dunia leo saa 10 jioni katika Hosptali ya TMJ Mikocheni.
Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es salaam.
"Ni kweli mzee amefariki dakika 50 zilizopita, alikuwa nyumbani amekaa lakini sukari ilishuka ghafla na baadaye kidogo alifariki" amesema Jerry Komba mtoto wa marehemu.
Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper Tumaini amesema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ ambapo ndipo mauti yamemkuta.
Aidha Bwana Gaspaer Tumaini ameongeza kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa katika hosptali ya Lugalo jijini
Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi itatangazwa baadaye
YANGA YASONGA MBELE LICHA YA KUFUNGWA NA BDF
Dk 29,
Ngassa analiifungia Yanga bao safi kwa kichwa cha kuchupa baada ya basi
nzuri ya Amissi Tambwe aliyeuwahi mpira alioutema kipa wa BDF.
Kipindi
cha pili BDF XI walirudi na moto na kufanikiwa kuwabana Yanga na
kurudisha bao na kuongeza la pili lakini na matokeo
kusomeka mwisho wa mchezo 2-1.
Kwa kuwa Yanga wanafaida na bao la ugenini na pia
ushindi wa 2 bila majibu walioupata Tanzania katika mchezo wao wa
Tanzania uliwahakikishia kuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano.
Kwa hiyo kwa matokeo hayo Yanga wanasonga mbele kwa kuwa na magoli 3
kwa mawili ya BDF XI.
Habari zilizotufikia hivi punde timu hiyo itarejea kesho kupitia Nairobi
Agriculture
-
Soil has vital nutrients for plants. As a result, it is used in agriculture to nourish plants. The roots of a plant receive nutrients from the soil to help it grow. The North Carolina Department of Agriculture and Consumer Services notes that 13 essential plant nutrients come from the soil.
Building
-
Soil is an important part of the building process. Soil compaction, which increases the density of the soil, is done as part of the building process. The purpose of the compaction is to improve the load support. If not done, structural failure can result. Soil can also be used as building materials such as adobe and red bricks.
-
Pottery
-
Clay soil is used in making ceramics, or pottery. When water is added to clay soil, it can be used to create the ceramics. Once formed, you can leave it to dry and it will retain its shape. Any type of ceramic can be created with the clay soil, such as a vase, bowl, cup or sculpture.
Medicine
-
Soil is commonly used in antibiotics. Microbes created in the soil are harmful to bacteria, which is why soil is used in medicine. Medicines created by soil include skin ointments, tuberculosis drugs and anti-tumor drugs.
Beauty Products
-
Some beauty products are made with soil. Commonly used beauty products where used soil is used in the production include blush and foundation. Soil rich in clay can also be used in facial masks and toothpastes.
Read more : http://www.ehow.com/info_10057531_5-uses-soil.html
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)



