Jumamosi, 28 Februari 2015

AZAM NJE LIGI YA MABINGWA YACHEZEA KICHAPO CHA 3-0

AZAM YANG’OLEWA CAF, YACHAPWA 3-0

Azam FC imeng’oka katika michuano ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa El Merreikh.
Azam FC ilishinda kwa mabao 2-0 jijini Dar, hivyo kufanya ing’oke kwa jumla ya mabao 3-2.
Katika mechi iliyochezwa leo jijini Khartoum, Sudan, Azam FC ilianza kukubali bao katika dakika ya 11 mfungaji akiwa Coffie.

Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza na ilikuwa ni kuhakikisha Azam wanakomaa hadi mwisho, lakini ikashindikana.
Merreikh ilipata mkwaju wa penalti kutokana na faulo ya Serge Wawa, lakini ikakosa.
Baada ya hapo, mambo yalionekana kuwa magumu kwa Azam FC katika kipindi cha pili ambayo ilitaka kujilinda zaidi.
Dofr akaifungia Merreikh bao la pili katika dakika ya 85, Mkenya Allan Wanga aliyeingia kipindi cha pili, akafunga bao la tatu katika dakika ya 90 na kuimaliza Azam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni