Jumatano, 31 Mei 2017

Watafiti: Uendeshaji baiskeli za abiria hatarini kutozaa

Mhudumu wa bodaboda Bwaise, Kampala nchini Uganda mwaka 2008
Kijana akisubiri abiria kwa kutumia baiskeli katika biashara ya uchukuzi wa abiria.


Watafiti nchini Kenya wanasema kunaweza kuwa na changamoto nyingine - kwamba wahudumu wa kubeba abiria kwa baiskeli maarufu kama bodaboda nchini Kenya wanakabiliwa na hatari ya kupoteza uwezo wao wa uzazi.
Baada ya kufanya utafiti, waligundua kwamba waendeshaji boda boda walikuwa katika hatari ya kutoweza kutanua mishipa ya damu kwenye uume wakati wa kushiriki tendo la ngono.
Mmoja wa watafiti hao Isaac Wamalwa ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta aliambia BBC kwamba suluhu huenda likawa ni kutumiwa kwa kiti maalum ya waendesha baiskeli ambayo hakitadhuru uume wa waendeshaji.
Bw Wamalwa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya ya uzazi alifanya utafiti miongoni mwa vijana eneo la Bungoma, magharibi mwa Kenya.
Walichunguza wahudumu 115 wa boda boda wa umri wa chini ya miaka 40 eneo hilo, wakishirikiana na wataalamu wa afya ya uzazi kutoka Hospitali ya Taifa ya Kenyatta na Chuo Kikuu cha Nairobi.
"Tuliwachunguza vijana waendeshaji wa bodaboda Bungoma na matokeo yalikuwa ya kushangaza. Kwa jumla, tuligundua kwamba zaidi ya theluthi moja ya waendeshaji bodaboda, asilimia 35.9, ya washiriki walikuwa na matatizo ya kuweza kusimika," aliambia gazeti la Standard la Kenya.
Anasema tatizo lilitokana na kuendesha baiskeli hizo kwa muda mrefu.
Bw Wamalwa anasema wote walioendesha baiskeli kwa zaidi ya saa 60 kwa wiki, walikuwa na matatizo ya kiafya.
Anatahadharisha pia kwamba maelfu ya vijana wanaofanya mazoezi kwenye vituo vya mazoezi mijini, kwa Kiingereza gym, ambapo huendesha baiskeli zisizo na gia, wanakabiliwa na hatari sawa na hiyo.
"Ujumbe wetu ni muhimu kwao pia, kwamba wanafaa kuwa wanapumzika kwa muda kutoka kwa kazi yao. Anasema wanapojikakamua kutafuta posho, wanafaa pia kujali uwezo wao kitandani.
Wataalamu wengine sita kutoka Chuo Kikuu cha Moi walifanya utafiti mjini Eldoret, magharibi mwa Kenya, na kupata matokeo yanayokaribiana na ya Bw Wamalwa.
Waliwachunguza wahudumu wa dbodaboda 131 wa umri wa kati ya miaka 18 na 65, umri wa kadiri ukiwa miaka 40.
Waligundua kwamba asilimia 76 kati yao walikuwa na matatizo kitandani.
Watafiti hao pia walidokeza kwamba tatizo hilo huenda linatokana na kuendesha baiskeli kwa muda mrefu.

Alhamisi, 25 Mei 2017

Wakongwe waliozoea kufanya kazi duniani hawa hapa





Prince Philip
  Mwanamfalme Philip anasema atajiuzulu baadaye mwaka huu

Wakati Mwanamfalme Philip, anafikisha miaka 96 mwezi Juni anastaafu majukumu yake ya kifalme baadaye mwaka huu, tunawaangazia baadhi ya watu wanaofurahia kazi zao kiasi cha kuamua kuendelea kufanya kazi - wengi wao hata kumpita Kiongozi huyo wa Edinburgh.
David Goodall, Mwansayansi mkongwe Australia
Mkongwe huyo wa miaka 103 mwaka jana alishinda kesi kuendelea kufanya kazi katika chuo kikuu kilichoko magharibi mwa Australia cha Edith Cowan huko Perth.
Dr Goodall aliagizwa kufanya kazi akiwa nyumbani 2017 huku kukiwa na wasiwasi kuhusu usalama wake, lakini chuo hicho baadaye kilisema, nafasi nzuri imepatikana katika tawi la chuo hicho lililoko karibu na makaazi ya mwanasayansi huyo.

Jumanne, 23 Mei 2017

MASHOGA WAPO? Wanaume waliofumaniwa wakifanya mapenzi Indonesia wamechapwa viboko 85 kila mmoja

 Wanaume waliofanya mapenzi wachapwa vikobo 85 Indonesia
Wanaume waliofanya mapenzi ya jinsia moja wakichapwa vikobo 85 Indonesia
Wanaume wawili wamechapwa viboko 85 kila mmoja kwenye mkoa wa Ace nchini Indonesia baada ya kufumaniwa wakifanya mapenzi.
Wanaume hao walisimama kwenye jukwaa wakiwa na mavazi meupe wakiomba, huku kundi la wanaume likiwachapa vikobo kwenye migongo yao
Indonesia imeharamisha mapenzi ya Jinsia moja na Mkoa wa Acheh hutawaliwa na sheria ya kidini- Sharia.
Adhabu hiyo ilitolewa mbele ya umma.

BREAKING NEWZZZZ: Watu 22 wauawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza

 Manchester explosion
Watu 22 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza
Polisi katika mji wa Manchester nchini Uingereza wanasema watu 22 wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa kwenye mulipuko uliotokea ndani ya ukumbi wa tamasha la muziki.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha ugaidi. 

Ikiwa itathibitishwa kuwa ni shambulio la kigaidi, litakua mbaya zaidi kuwahi kukumba Uingereza tangu Julai mwaka 2005 wakati zaidi ya watu 50 walikufa kwenye misururu ya milipuko mjini London.

Jumapili, 21 Mei 2017

WABAKAJI SOMA HII: Mwanamke akata uume wa kiongozi wa dini mbakaji India

Siku ya Ijumaa usiku alichukua kisu na kumshambulia wakati alijaribu kumbaka na kisha kuwaita polisi mwenyewe.

Mwanamke mmoja wa umri wa miaka 23 nchini India amekata uume ya wa kiongozi mmoja wa dini kwenye jimbo lililo kusini mwa nchi la Kerala, akidai kuwa alimbaka kwa miaka kadhaa.
Polisi wanasema kuwa kiongozi huyo wa dini kwa jina Gangeshananda Theerthapada, alikuwa akienda kwenye nyumba ya mwanamke huyo kufanya maombi kwa ajili ya afya ya babake.
Hii ni baada ya mama yake kuwa na matumaini kuwa mtu huyo ya Mungu angetatua matatizo ya familia yake.

Badala yake binti yake alidai kuwa alimdhulumu kingono kila mara.
Siku ya Ijumaa usiku alichukua kisu na kumshambulia wakati alijaribu kumbaka na kisha kuwaita polisi mwenyewe.
 Mwanamke akata uume wa kiongozi wa dini India
Mtuhumiwa huyo wa ubakaji kisha akakimbizwa hospitalini kwa matibabu ya dharura.
Hospitali hiyo ilisema mwanamume huyo wa miaka 54 kutoka Kollam alilazwa kwenye hospitali hiyo 

Uume wake ulikuwa umekatwa kwa asilimia 90 na hakuna uwezekano kuwa ungerudishwa tena. Madaktari walijaribu kuzuia kufuja kwa damu na kumfanyia upasuaji ili aweze kupitisha mkojo.

Alhamisi, 18 Mei 2017

Baraza lapinga pendekezo la saa moja ya ngono Sweden

Per-Erik Muskos, diwani wa Övertorneå alipendekeza kuwapatia wafanyikazi hao mapumziko ya saa moja kila wiki

Per-Erik Muskos, diwani wa Övertorneå aliyependekeza kuwapatia wafanyikazi hao mapumziko ya saa moja kila wiki 
 
Madiwani katika baraza la mji mdogo wa Sweden wamepinga muswada wa pendekezo la kuwapa wafanyikazi wa manispaa, 'mapumziko ya kufanya tendo la ngono'
Per-Erik Muskos, diwani wa Övertorneå alipendekeza kuwapatia wafanyikazi hao mapumziko ya saa moja kila wiki kwenda nyumbani na kupata wakati bora wa kujamiana na wapenzi wao.
Aliiambia BBC kuwa lengo kuu lilikuwa kuimarisha uhusiano baina ya watu.
''Ni jina la herufi tatu{Sex} , ''Bw Muskos aliposema mwezi Februari, akipuuza wazo la kwamba anaingililia maisha ya watu binafsi.
Lakini wanachama wa baraza hilo ambao ni wahafidhina walipinga wazo hilo.
Meya wa Övertorneå, Tomas Vedestig, alihitimisha kwa kusema maisha ya kibinafsi ya wafanyakazi yanastahili kuwachwa vile yalivyo.
''Si kazi ya baraza kuingilia,'' aliambia SVT.
Bw Muskos alitumai kwamba kichwa cha mpango wa huo ungeongeza idadi ya watu katika mji wake ambao kwa hivi sasa idadi hiyo imezidi kushuka.
Mji wa Övertorneå kwa hivi sasa ni eneo ambalo lina watu 4,500 lakini wengi wao ni mwenye umri wa wastani.
''Vijana wengi huondoka mji huo pindi tu wanapokamilisha masomo yao, diwani huyo amesema.
Pia anadhani kwamba kutenga saa moja kwa wiki kutawasaidia wanandoa ambao hawana wakati na wapenzi wao.
''Watu wana vitu vingine vingi vya kufanya ,'' alisema. Ukiwa nyumbani watu wako kwenye mitandao, unahitajika kuwapeleka watoto kushiriki katika michezo ya soka na mpira wa magongo ya barafu, watu hawana muda .
Iwapo wafanyikazi wa 550 wa baraza wamekasirika, itakuwa nzuri  ya kutoa hasira katika hali hiyo mbaya: kwa sasa watumishi hao wana saa moja kwa wiki kushiriki katika michezo tofauti.

NANI KASEMA ELIMU INA MWISHO: Waziri Mkuu wa zamani afaulu mtihani akiwa na miaka 82 India

Bw Chautala alihudumu kama waziri mkuu wa jimbo la Haryana kaskazini mwa India kwa mihula minne

 Bw Chautala alihudumu kama waziri mkuu wa jimbo la Haryana kaskazini mwa India kwa mihula minne
Waziri wa zamani ambaye anatumikia kifungo gerezaji baada ya kupatikana na kosa la kula rushwa amefaulu mtihani wa kumaliza shule India akiwa na miaka 82.
Om Prakash Chautala, aliyehudumu kama waziri mkuu wa jimbo la Haryana kaskazini mwa India kwa mihula minne, alifanya mtihani wa darasa la 12 akiwa katika jela ya Tihar mjini Delhi.
Mwanawe wa kiume Abhay Chautala alisema babake aliamua "kutumia vyema muda wake gerezani".
OP Chautala alipatikana na makosa kuhusiana na kuajiriwa kwa walimu.
Abhay Chautala aliambia gazeti la Indian Express kwamba babake amekuwa kila siku akienda kusoma katika maktaba ya gereza hilo.
"Husoma magazeti na vitabu. Huwa anawaomba wafanyakazi wa jela kumtafutia vitabu avipendavyo zaidi. Husoma vitabu kuhusu wanasiasa maarufu duniani, amesema.
Bw Chautala na 54 wengine, walipatikana na hatia ya kughushi vyeti walipokuwa wanawaajiri walimu 3,206 kati ya 1999 na 2000.
Waendeshaji mashtaka walisema watu waliokuwa wamehitimu zaidi walikataliwa na badala yake wale waliokuwa wametoa hongo wakaajiriwa.
Bw Chautala ni kiongozi wa chama cha Indian National Lok Dal Party na ni mwana wa aliyekuwa naibu waziri mkuu Devi Lal.

UKSHANGAA YA NANIHII UTAONA YA .... Kijana aliyejaribu kumbusu nyoka aumwa usoni Marekani

Nyoka huyo anaaminika kutokeka baada ya kisa hicho.

Nyoka huyo anaaminika kutoweka baada ya kisa hicho.

Mwanamume mmoja katika jimbo la Florida nchini Marekani ambaye alijaribu kumbusu nyoka na badala yake nyoka huyo akamuuma, anaendelea kupata matibabu hospitalini.

Nyoka huyo aliokotwa na Charles Goff, mkazi wa kaunti ya Putnam kaskazini mwa jimbo la Florida siku ya Jumatatu.

Siku moja baadaye jirani yake ambaye alitajwa na kituo cha CBS kama Ron Reinold alianza kucheza na nyoka huyo kwa kujaribu kumbusu.

Bwana Reinold alisafirishwa kwa njia ya ndege na kwa sasa anaendelea kupata nafuu hospitalini,.

Kijana mmoja alisema, "nitambusu mdomoni," ndipo nyoka huyo akamuuma usoni, bwana Goff alililiambia shirika la habari la Action News Jax.

Kituo cha First Coast News kilisema kuwa muathirika alikuwa na fahamu lakini katika hali yake ilikuwa mbaya. Nyoka huyo anaaminika kutoweka baada ya kisa hicho.

Haijulikani sababu iliyochangia bwana Reinold ajaribu kumbusu nyoka huyo.

Jumanne, 16 Mei 2017

Mfungwa aomba adhabu ya kifo cha kumiminiwa risasi Marekani

JW Leford amekuwa akitumia dawa ya kupunguza maumivu ya nevi ambazo mawakili wake wanasema huenda zikabadili utendakazi wa ubongo wake

 JW Leford amekuwa akitumia dawa ya kupunguza maumivu ya nevi ambazo mawakili wake wanasema huenda zikabadili utendakazi wa ubongo wake.
 
Mfungwa mmoja anayesubiri kunyongwa katika jela moja katika jimbo la Georgia nchini Marekani amewasilisha ombi la kuuawa kwa kuumiminiwa risasi kwa sababu kifo cha kuuawa kwa kudungwa sindano kina uchungu mno.
JW Leford amekuwa akitumia dawa ya kupunguza maumivu ya neva ambazo mawakili wake wanasema huenda zikabadili utendakazi wa ubongo wake na kumfanya kuwa na uchungu mkali kinyume na katiba.
Ledford alihukumiwa 1992 kwa kumuua jirani yake.

DUNIANI KUNA MAMBO: Mwanamke ajioa baada ya kukosa mchumba

Q May Chen Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa

May Chen Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa
Mwanamke mmoja ambaye anaugua saratani ya matiti amejioa mwenyewe baada ya kusubiri mchumba kwa muda mrefu.
May Chen mwenye umri wa miaka 28 kutoka Taiwan ameambia BBC kwamba anaugua ugonjwa huo lakini hajakubali sababu hiyo kuhujumu ndoto yake ya kuolewa.
''Nimekuwa nikisubiri mtu kujitokeza na kusema kwamba angependa kufunga ndoa nami mbali na kupiga picha za harusi nami aliambia BBC .
Anasema kwamba wakati unapohisi kwamba huna miaka mingi ya kuishi huna budi kujifanyia maswala ambayo yamekuwa ndoto yako.
Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa.