Jumatano, 18 Aprili 2018

Nape Nnauye Ahoji Kuhusu Soko la Mbaazi Bungeni.......Serikali Yajibu Soko ni Baya, Watanzania Waitumie Kula Maana ni Chakula Kizuri


SeeBait
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameuliza serikali imefikia wapi kutafuta soko la Mbaazi baada ya msimu uliopita matatizo ya soko kushusha bei kutoka Tshs 2,000 mpaka 150. Amesema serikali iliahidi Bungeni kuwa itahakikisha inahangaika kupata soko la kuaminika la zao hilo.

Nape amesema sasa ni msimu wa kilimo hicho, kama bado hali haieleweki wananchi washauriwe waachane na mbaazi na badala yake wajikite kwenye mazao mengine ambayo yana soko la uhakika.

Akijibu swali hilo naibu waziri wa kilimo, Eng. Stella Manyanya amemjibu kuwa ni kweli hakukuwa na hali inayoridhisha kwenye soko la mbaazi na ni kutokana na wadau waliokuwa wanategemewa sana ilikuwa ni India.

Neema yaja kwa watumishi wa umma


SeeBait
SERIKALI imetangaza neema kwa watumishi wa umma 4,812 baada ya jana kubainisha kuwa kuna fursa za mafunzo 659 zitakazotolewa na Serikali ya China.

Fursa hizo za mafunzo zimejikita kwenye maeneo ya kipaumbele cha taifa yaliyoainishwa katika Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21).

Katika mkutano wake na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari na Elimu ya Bunge mjini hapa jana, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema mafunzo yamejikita kwenye uhandisi wa viwanda, mawasiliano na usafirishaji.

Dk. Ndumbaro pia alisema mafunzo hayo yatajikita kwenye kilimo, elimu, afya, biashara na uchumi, Tehama na utawala bora.

Serikali Kuajiri Walimu 6,000 June


SeeBait
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imesema hadi kufikia Juni 30 mwaka huu inatarajia kuajiri walimu 6,000 wa masomo ya Hisabati na Sayansi kwa ajili ya shule za sekondari nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Joseph Kakunda, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali, ambaye alitaka kujua mikakati ya serikali katika kuondoa changamoto katika shule za kata ikiwamo upunguzu wa walimu wa Hisabati na Sayansi.

Pia, Bobali alitaka kujua msimamo wa serikali kuhusu wananchi kuchangia kwenye chakula ambacho wameona ndio chachu ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi katika Mkoa wa Lindi. Alisema hadi Desemba mwaka 2017, Serikali ilikuwa imeajiri walimu 200 wa Hisabati na Sayansi kwa ajili ya shule za sekondari.

Kadhalika, alisema serikali haijazuia wananchi kuchangia maendeleo ya shule walichokataza ni kumzuia kumpa adha ya kukosa masomo mwanafunzi ambaye ameshindwa kuchangia michango hiyo.

AJIRA ZA UTUMISHI WA UMMA 2017- 2018

Cheki www.mabumbe.com

Alhamisi, 11 Januari 2018

Bendera: Tanzania na Korea Kaskazini zazozana

 

Tanzania imefutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria.Tanzania imefutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria.                
Taifa la Tanzania limefutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria.
Waziri wa maswala ya kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga aliambia BBC kwamba meli hizo zilionekana hivi karibuni katika bahari hindi eneo ambalo halipo mbali na Tanzania.
Hatahivyo hakutoa idadi kamili ya meli hizo.
''Meli za Korea Kaskazini zilipigwa marufuku na Umoja wa Mataifa na hazikuruhusiwa kusafiri ama hata kutia nanga'',alisema Mahiga.
''Kwa hivyo meli hizi zimekuwa zikijaribu kutafuta njia kukiuka vikwazo hivyo ili kuweza kuendelea na biashara zao,na mbinu moja ni kupeperusha bendera za mataifa tofauti''.
Waziri huyo amesema kuwa malalamishi yametumwa katika serikali ya Korea Kaskazini wakilaumu biashara hiyo ya ujanja.
''Shirika la kimataifa la maswala ya baharini pia limeelezewa ili kuwakamata wamiliki wa meli hizo'',aliongezea Mahiga.

Meli yenye bendera ya Tanzania yanaswa Ugiriki ikipeleka vilipuzi Libya

 

Tanzania imefutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria.                   Mwaka 2016, Tanzania ilifutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria                
Maafisa wa Ugiriki wanaoshika doria baharini wamesema wanaizuilia meli iliyokuwa inapeperusha bendera ya Tanzania ambayo ilikuwa imebeba vilipuzi.
Meli hiyo inadaiwa kusafirisha vilipuzi hivyo kutoka Uturuki kwenda Libya, kinyume na marufuku iliyowekwa ya kutosafirisha silaha kwenda Libya.
Maafisa wanasema meli hiyo ilikuwa imebeba kreti 29 zilizojaa vilipuzi pamoja na kemikali zinazotumiwa kuunda vilipuzi ikiwemo.
"Maafisa wa kushika doria baharini wamezima bomu lililokuwa linasafiri," afisa mkuu wa walinzi hao wa Ugiriki Yiannis Sotiriou aliwaambia wanahabari, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ANA.
Wizara ya Safari za Baharini ilisema meli hiyo ilisimamishwa ikiwa katika kisiwa cha Crete kusini mwa Ugiriki wikendi baada ya maafisa kupashwa habari na mdokezi.

Ilisindikizwa hadi katika bandari moja kisiwa hicho cha Crete na kufanyiwa ukaguzi.
Crete
Sotiriou alisema meli hiyo ambayo ilinaswa Jumamosi ilikuwa pia na kasoro nyingi na haikufaa kuwa baharini.
"Ingesababisha madhara makubwa sana kwa watu na mazingira pia," amenukuliwa na AFP.
Nahodha wa meli hiyo kwa jina Andromeda alidai ilikuwa inasafiri kuelekea Djibouti lakini baadaye ikabainika kwamba ilikuwa inasafiri kuelekea mji wa bandarini wa Misrata nchini Libya.
Shirika la AFP linasema mabaharia hao wanane waliokuwa kwenye meli hiyo watafikishwa mbele ya mwendesha mashtaka leo.
Watano kati ya mabaharia hao ni raia wa India, wawili wa Ukraine na mmoja wa Albania.

Jumatano, 10 Januari 2018

Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda

Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda

              Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda
Mfugaji mmoja wa nguruwe kaskazini mwa Rwanda amepata siri ya aina yake kuwafanya nguruwe anaofuga kuongeza uzalishaji.
Siri hiyo ni muziki unaotumbwiza saa 24 katika mazizi yao.
Mfugaji huyo maarufu Sina Gerald anasema muziki huwasaidia nguruwe kunona, kujifungua vizuri na kutumia chakula kidogo ikilinganishwa na nguruwe wasiosikia muziki.
Mzee Theophile Hakizimana ambaye ni mpokezi ya wageni shambani anasema kuna aina mbili za nguruwe, Landras ambao ni nguruwe warefu na Large White ambao ni wafupi lakini wanono.
Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda
                             Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda
Ana nguruwe wapatao 700 pamoja na chakula cha kawaida , nguruwe hawa hupata muziki saa 24.
"Muziki huu unasaidia nguruwe kuwa watulivu,kuwa na afya nzuri,na pengine niseme kuwa nguruwe wanatoa uzalishaji mwingi wakati wanapata muziki kama huu" anasema Hakizimana.
Anasema kwa muda mrefu wamekuwa wakiendesha utafiti kuhusu nguruwe na uzalishaji wao kwa ujumla
Kuna pia faida kubwa kwa mfugaji kwa sababu Nguruwe wakipata muziki kama hivi wanakula chakula kidogo sana ukilinganisha na nguruwe ambao wanakula bila kusikia muziki.
Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda
                                   Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda
"Hapa nalinganisha na chakula tunachowapa nguruwe wengine tulionao ambao wao hawapati muziki. Hii ni kwa mjibu wa utafiti tuliofanyia nguruwe katika kituo chetu''
Ufugaji wa nguruwe umeshika kasi nchini Rwanda kutokana na faida yake ya haraka kibiashara.
Nyama ya nguruwe ndiyo ghali kuliko nyama nyingine sokoni. Kilo moja ikiwa ni franga si chini ya elfu 4 za Rwanda kama dolla 5.
Kitoweo cha nguruwe ni miongoni mwa vitoweo vyenye mvuto wa hali ya juu kwenye vilabu vya pombe katika majiiji ya Kigali na Kampala kikifahamika kwa jina maarufu ''Akabenz''

Mwanamume achoma moto nyumba akiua buibui California, Marekani

    

A wolf spider at Sydney Wildlife World on July 18, 2008.                  Buibui huyo anaaminika kuwa buibui mkubwa aina ya 'wolf spider'                
Mwanamume mmoja katika mji wa Redding kaskazini mwa California, Marekani anadaiwa kuchoma moto nyumba akijaribu kumuua buibui.
Kisa hicho kilitokea Jumapili kwa mujibu wa vyombo vya habari Marekani.
Mmoja wa walioshuhudia, ambaye alikuwa anaishi katika nyumba hiyo kubwa ya makazi, ameambia gazeti moja California kwamba buibui huyo huenda alichangia kueneza moto huo chumbani, akikimbia akiwa anaungua.
Haijabanika iwapo buibui huyo alinusurika.
Hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa, lakini wakazi wa jumba hilo walioondolewa salama.

Afisa wa idara ya zimamoto eneo hilo Gerry Gray ameambia BBC ni kwenye kwamba moto ulizuka katika jumba hilo lakini akasema chanzo cha moto huo bado kinachunguzwa.
"Taarifa kuhusu 'buibui' zilitolewa na raia walioshuhudia, waliokuwa eneo la tukio, na bila shaka zinatumiwa katika uchunguzi.
Buibui huyo alikuwa aina ya 'wolf spider' ambao ni buibui wakubwa.
Idara ya zima moto imeambia gazeti la Redding Record Searchlight kwamba dalili zinaonesha moto huo uliwashwa na mwenye nyumba.
California map
Redding, eneo ambalo kisa hicho kilitokea, ni mji ulio maili 162 (261km) kaskazini Sacramento.
Walioshuhudia wanasema buibui huyo alieneza moto alipokimbia na kujificha kwenye mto.
Mto huo ulishika moto na moto huo, na ingawa wakazi waliweza kuuzima hapo, ulikuwa tayari umeenea maeneo mengine ya jumba hilo.

Maafisa wanasema moto huo ulisababisha uharibifu wa takriban $11,000 (£8,000) na baadhi ya vyumba vya jumba hilo vitahitaji kukarabatiwa kabla ya watu kuishi huko tena.
Hiyo ni hasara ya kuogopa vitu hata kama havina madhara ambayo kwa kiingereza huitwa "phobia" ambapo watu huogopa hata chura, kinyonga, jongoo nk

Jumatatu, 8 Januari 2018

Meli inayoteketea baharini hatarini kulipuka na kuzama

     

Oil tanker on fireMeli inayoteketea baharini iko katika hatari ya kulipuka na kuzama                
Kuna hofu kubwa ya kutokea janga la kimazingira Kusini mwa bahari ya China wakati meli ya kubeba mafuta inazidi kufuja siki mbili baada ya kugongana na meli nyingine ya mizigo.
Maafisa nchini China wameviambia vyombo vuya habari kuwa meli hiyo iko kwenye hatari ya kulipuka na kuzama.
Wakoaji wanaojaribu kufika eneo hilo wanazuiwa na moshi mkubwa.
Wahuhudumu 30 raia wa Irana na 2 wa Bangladesh bado hawajulikani waliko licha ya jitihada za kimataifa kuwaokoa.

Kiwango cha uchafuzi wa mazingira bado hakijulikani. Chombo hicho bado kilikuwa kinateketea leo Jumatatu.
Licha ya kuwa na usajili wa Panama meli hiyo inamilikiwa na kampuni ya Iran.
Sanchi ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta ya Iran wakati iligongana na meli ya mizigo ya China Jumamosi usiku.
Wahudumu 21 wa meli ya mizigo ya China waliokolewa.
Map
        Wahudumu 30 raia wa Irana na 2 wa Bangladesh bado hawajulikani waliko licha ya jitihada za kimataifa kuwaokoa.            
Watu wanaoshughulikia mazingara mnasemaje?    

Njia za kukabiliana na upara

Mwanamume mwenye upara

Tatizo la kunyonyoka kwa nywele na kuwa na kipara limekuwa likiwatatiza wanaume wengi kwa muda.
Shida hii mara nyingi huanza wanaume wakiwa wana miaka 30 hivi, na kufikia umri wa miaka 50 ambapo nusu ya wanaume huwa wanakabiliwa na tatizo hili.
Tatizo hili hutokana na vinyweleo vya nywele, ambavyo huwa kina cha ukuaji wa nywele, kunywea. Shughuli hii huendelea pole pole kwa muda mrefu.
Kuna wengi wanaodai kuwa na tiba ya tatizo hili, baadhi wakitumia dawa za kisasa na wengine za kiasili lakini ufanisi wake huwa tofauti.
Ni njia gani hufanikiwa?
Kwa mujibu wa Idara ya Taifa ya Afya Uingereza (NHS) kupandikizwa kwa nywele ni moja ya njia zinazofanikiwa sana.
Lakini gharama yake huwa ya juu mno.
Kupandikizwa nywele kunaweza kugharimu kuanzia £1000 hadi £30,000 [sawa na shilingi za kitanzania milioni 3 hadi 90].
Wakati mwingine, daktari wako anaweza kupendekeza utumie dawa yenye kiungo fulani ambacho hujulikana kama Finasteride. Kiungo hiki hubadilisha viwango vya homoni fulani zinazodhibiti mfumo wa uzazi katika binadamu.
Utafiti unadokeza kwamba tiba hii inaweza kusisimua ukuaji wa nywele tena katika theluthi mbili ya wanaume wenye upara.

Dawa nyingine kwa jina Minoxidil iligunduliwa kibahati miaka ya 1950 watafiti waliokuwa wanatafuta tiba ya shinikizo la damu. Inaaminika kwamba hufanya kazi kwa kwa kuongeza mtiririko wa damu kwenye ngozi ya kichwa maeneo yenye nywele na kufungua vinyweleo vya nywele.
Ikitumiwa vyema, inaweza kufanikiwa kwa asilimia 80 ya wanaoitumia, lakini huhitaji kutumiwa kwa muda mrefu.
Kutumia dawa hizi mbili kunaweza kukugharimu maelfu ya pesa kila mwaka.



Kuna ushahidi pia kwamba aina fulani ya vyakula vina uwezo wa kuzuia upara. Kuna utafiti ulioonyesha kwamba ulaji wa vyakula vyenye Omega 3 kwa wingi ulipunguza kunyonyoka kwa nywele pole pile.
Upara huhusishwa pia na upungufu wa madini ya chuma mwilini, hivyo kula mboga zenye rangi ya kijani (mfano spinachi) kunaweza pia kumfaa mtu.
Kando na kula vyakula vifaavyo, utafiti unadokeza pia kwamba kufanya mazoezi zaidi na kupunguza mfadhaiko ni mambo yanayoweza kupunguza kunyonyoka kwa nywele pia.