Jumatano, 27 Novemba 2013

ZITTO AMSHITAKI HENRY KILEWO POLISI KWA KUSAMBAZA WARAKA ONLINE



WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikimwandikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe barua ya kumtaka ajieleze dhidi ya tuhuma zinazomkabili, yeye ameamua kukimbilia polisi akimshitaki mmoja wa viongozi wenzake.
Habari za kuaminika zimedai kuwa Zitto ambaye hivi karibuni alivuliwa cheo chake cha unaibu katibu mkuu wa CHADEMA, inadaiwa amefungua mashitaka polisi akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii.
Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.

Ijumaa, 15 Novemba 2013

Ni hali ya kusikitisha Ufilipino

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufilipino, ameambia BBC kuwaidadi kamili ya watu waliojeruhiwa kutokana na Kimbunga Haiyan, wiki jana, imefika watu elfu tatu na mia tano.
Bwana Mar Roxas amekiri kuwa idadi hiyo hata hivyo huenda ni kubwa zaidi ya hiyo.

Ingawa idadi rasmi ya waliofariki bado haijulikani na maafisa katika moja ya majimbo yaliyoathirika zaidi kuliko yote, wanasema kuwa watu elfu nne wamefariki jimboni humo pekee.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa serikali italazimika sasa kuanza kufanya mipango ya ujenzi mpya na wa kudumu.
Serikali inakadiria uharibifu uliotokea kuwa wenye thamani ya dola bilioni 15.
Asilimia tisini ya nyumba zimeharibika na maelfu ya shule haziwezi tena kutumika.
Watoto hawaendi tena shule hadi mwezi Januari.2014.
Wakati huohuo, wafanyakazi wa kutoa misaada nchini wametaja hali iliyoko nchini humo kama ya kusikitisha, wiki moja tu baada ya kimbunga Haiyan kupiga maeneo ya kati ya nchi hiyo. Maelfu ya raia wa nchi hiyo bado wanahitaji misaada ya dharura.
Msemaji wa shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka, la Medicins sans Frontiers, Henry Gray, amesema masuala mengi ya mipango yanaathiri shughuli ya kusambaza misaada.
Katibu mkuu wa muungano wa nchi wanachama wa muungano wa asia na pacific ASEAN Lee lair-un min amesema misaada zaidi itatolewa na kuwa mataifa yote duniani yanaweza kufanya mengi zaidi kusaidia.

Hawa ndio mabilionea wanne vinara Tanzania

Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz (49), ametajwa kuwa ndiye tajiri namba moja Tanzania kwa sasa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la Marekani la Forbes na kutoa taarifa yake juzi, Rostam amekamata nafasi hiyo na ya 27 katika Afrika akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni moja (Sh1.6 trilioni).
Mbunge huyo wa zamani wa Igunga, ameingia kwa mara ya kwanza katika orodha ya matajiri 50 wa Afrika ya jarida hilo, pamoja na wafanyabiashara wengine wa Tanzania, Reginald Mengi na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohamed Dewji ‘Mo’. Katika orodha hiyo pia yumo Said Bakhresa ambaye aliwahi kutajwa siku za nyuma.
Rostam, ambaye aliachana na siasa mwaka 2011, amempiku Bakhresa, ambaye mwaka jana Jarida la Ventures Africa la Nigeria lilimtaja kuwa ndiye aliyekuwa tajiri namba moja wa Tanzania. Bakhressa katika kipindi hicho alikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 620 milioni (Sh971 bilioni).
Katika orodha hiyo ya Ventures Africa, Bakhresa alifuatiwa na Rostam, Mengi na mfanyabiashara mwingine maarufu, Ali Mufuruki.
Mengi anashika nafasi ya pili kwa Tanzania na ya 34 Afrika akiwa na utajiri wa Dola 550 milioni (Sh861 bilioni).
Forbes linaonyesha kuwa Bakhresa amefungana na Mo katika nafasi ya tatu ya orodha ya matajiri wa Tanzania na ya 38 kwa Afrika, wote wakiwa na utajiri wa Dola 500 milioni (Sh783 bilioni).

LOWASSA AMMWAGIA SIFA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA KUTEKELEZA ILANI KWA KIWANGO KIKUBWA KULIKO AWAMU NYINGINE.



 

RAIS KIKWETE.
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, ameisifu Serikali ya Awamu ya Nne na kudai ndiyo iliyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kiwango kikubwa sana kuliko awamu nyingine zilizopita. 

Lowassa aliyasema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara baada ya kuweka jike la msingi la ujenzi wa hospitali ya kisasa wilayani humo na kusisitiza kuwa, ujenzi huo ni matokeo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.

KAMPUNI YA DELINA DGE YATOA VIFAA VYA MAMILIONI YA PESA KUSHINDANISHA UHURU CUP KWA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA MAREKANI

Mwakilishi wa kampuni ya Delina Group (DGE) kushoto,Bw. Emmanuel Mzava,akionyesha waandishi wa habari vifaa vya michezo vilivyotolewa na Bw. Davis Mosha. Kulia ni  Mkurugenzi wa Swahili Media International, MMK Media Group Bw. Alex Kassuwi (kulia).
Kampuni ya Delina Group (DGE) inayomilikiwa na Bw. Davis Mosha imekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya mamilioni ya pesa pamoja na vikombe kwa ajili ya kumtafuta Bingwa wa Uhuru Cup kwa timu za mpira ambazo zinaundwa na watanzania ambao wanaishi nchini Marekani na ni mashabiki wa Simba na Yanga. Tarehe za mechi hizo zitatajwa hivi karibuni tukishirikianana ubalozi wa Tanzania.

Jumanne, 5 Novemba 2013

MBUNGE ALIYEOLEWA NA KIJANA MDOGO ADAI KUWA KIJANA NDO KAMNG'ANG'ANIA



Hatimaye Mbunge Rosweeter Kasikila (60), aliyefunga ndoa na kijana mwenye umri wa miaka 26, amefunguka kwa kusema aliyeng'ang'ania kufunga ndoa hiyo ni kijana mwenyewe licha ya kumtahadharisha tofauti ya umri wao.
Kasikila alitoa kauli hiyo jana, baada ya kutakiwa kujibu shutuma zilizotolewa na mumewe huyo, Michael Christian (26) ya kung'ang’ania vyeti vyake vya elimu kwa lengo la kumtaka arudi nyumbani.
Christian aliyefika katika ofisi za NIPASHE jana alitoa nakala ya barua aliyoituma kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, kuomba atumie uwezo wake wa kisheria ili mbunge huyo amrudishie vyeti vyake alinavyovishikilia.

Kufuatia maelezo hayo, NIPASHE ilimtafuta Dk. Nchimbi kwa njia ya simu ili athibitishe kupokea nakala ya barua hiyo lakini simu yake ilikuwa imezimwa.

Nakala nyingine za barua hiyo zilitumwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Haki za Binadamu kwa jamii-Madhehebu ya dini nchini, Askofu William Mwamalanga, Mchungaji wa Kanisa la Assembilies of God, Mikocheni B, Mchungaji Getrude Rwakatare na vyombo vya habari.

Akijibu shutuma hizo, mbunge huyo alisema hajawahi kung'ang'ania vyeti vya kijana huyo wala kulazimisha ndoa kama anavyodai Christian.

MBUNGE WA KIGOMA ZITTO KABWE AFICHUA YA MOYONI JUU YA SAKATA LA KUKATAA POSHO ZA VIKAO VYA BUNGE, GODLESS LEMA AENDELEA KUMTUHUMU KUTUMBUA POSHO.

 
DAR ES SALAAM
VITA vya maneno kati ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe imefika pabaya.
Vita hiyo ya maneno iliyoanzishwa na Lema katika kikao cha wabunge wiki iliyopita kwamba Zitto anafanya unafiki kukataa posho, jana iliingia katika hatua nyingine baada ya mwakilishi huyo wa Arusha kumshushia tuhuma Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kwamba anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho nyingi kutoka mashirika mbalimbali ya kijamii nchini.

Jumatatu, 4 Novemba 2013

RAIS KIKWETE AAGA MWILI WA JAJI HILARY MKATE

jk2Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Jaji Mstaafu Hilary Mkate leo Oktoba 4, 2013 Kinondoni Dar es salaamjk3Rais Jakkaya Kikwete akimfariji Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva baada ya kuaga mwili wa marehemu Jaji Mstaafu
Hilary Mkate leo Oktoba 4, 2013 Kinondoni, Dar es salaam
PICHA NA IKULU

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMJULIA HALI DKT. SENGONDO MVUNGI ALIYELAZWA MUHIMBILI

MvungiMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Dkt. Mugisha Clement, aliyekuwa akimpa maelezo kuhusu alivyompokea Mjumbe wa Tume ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi, aliyelazwa  katika Kitengo cha Uangalizi Maalum (ICU) MOI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipokwenda kumjulia hali, kufuatia kujeruhiwa na majambazi usiku wa kuamkia jumapili huko nyumbani kwake maeneo ya Kibamba. Picha na OMR

MAGAZETI YA LEO