Kamanda wa Polisi Mkoani
Morogoro,Faustine Shilogile akizungumza na wanahabari (hawapo
pichani).
Hizi ndio baadhi ya Pipi
zilitolewa tumboni mwa Marehemu Khalid Kitala.
Baadhi ya Makachero wa
Polisi wakijadiliana jambo baada ya kuona Mwili huo.
Jeshi la Polisi mkoani
Morogoro limefanikiwa kukamata gari dogo aina ya Toyota Spacio likiwa limebeba
mwili wa mtu aliefari ambaye alitambulikwa kwa Jila la Khalid Kitala (47) na
kukutwa na kete kadhaa za Madawa ya Kulevywa tumboni.
Kamanda wa polisi mkoani
Morogoro, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa
walipata taarifa za kuwepo kwa gari hilo toka kwa wasamalia wema ambao
waliliona njiani, ambapo inasemekana lilikuwa linatokea Mkoani Mbeya kuelekea
Dar.
Polisi wa mkoa wa Morogoro
waliweka mtego wao kwenye kituo cha Mikumi na hatimaye kufanikiwa kukamata gari
hilo likiwa na watu watatu ndani (majina yao yamehifadhiwa),pipi saba za vitu
vinavyosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya.
Mwili huo ulipelekwa
hospitali na kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na pipi nyingine kumi na saba
tumboni mwa Marehmu huyo na inasemekana mtu huyo alifariki akiwa
Mbeya.
Watu wote watatu ambapo
wawili wanahusika na gari hilo na mmoja ni mfanyabiashara wa Kariakoo
wanashikiliwa na polisi huko Morogoro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni