Serikali imetangaza neema kwa vijiji vinavyopitiwa na bomba la gesi ambavyo vipo mkoani Mtwara na Lindi, sasa wataunganishiwa kwa Sh27,000.
Hatua hiyo ilitangazwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uzinduzi mradi wa umeme wilayani Nanyumbu na Masasi.
Profesa Muhongo alisema gharama za kuunganisha umeme kwa sasa ni Sh177,000.
Alisema zaidi ya vijiji 50 vimepewa upendeleo huo ili kuwawezesha wananchi kuwa na maisha bora.
Lengo la Serikali ni kufikia asilimia 30 ya wasasatu waliounganishwa na umeme na kwamba, hivi sasa ni asilimia 23 pekee wanaopata umeme nchini wakati Mtwara ni asilimia nne.
Kuhusu umeme wa gesi, Profesa Muhongo alisema Mtwara wanatarajia kuzalisha megawati 600 ambazo baada ya matumizi nchini, zitauzwa nchi za Malawi, Zambia na Msumbiji
Awali, akizungumza na mamia ya wakazi wa Mangaka waliofika kushuhudia uzinduzi huo, Pinda alisema mradi huo ni utekelezaji wa azma ya Serikali kuhakikisha kila wilaya inapata umeme.
"Mpango wa kupeleka umeme nchini ni wa miaka mitatu na katika sekta ya nishati chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Sasa (BRN), tumeazimia kwenda kwa awamu," alisema.
ili tuwafikie wananchi wengi zaidi kutoka asilimia 24 ya sasa hadi kufikia asilimia 30 ya watumiaji wa umeme," alisema Waziri Mkuu. Chanzo: mwananchi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni