Maafisa wakuu wa polisi nchini Nigeria, wanasema kuwa watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wenye itikadi kali za kiisilamu wametumia mabomu kushambulia kijiji kimoja Kaskazini mwa Nigeria na kuwaua watu wengi huku wakiteketeza nyumba zao.
Afisa mmoja wa usalama alisema Jumatatu kwamba waliofanya mashambulizi walitega mabomu katika soko moja katika kijiji cha Kawuri siku ya Jumapili.
Mmoja wa waliojeruhiwa alisema kuwa washambuliaji walikuwa karibu 50. Polisi mmoja aliyewaokoa majeruhi alithibitisha kuwa watu 52 waliuawa.
Afisa mmoja alilaumu kundi la wapiganaji la Boko Haram, ambalo limewaua maelfu ya watu katika kipindi cha miaka minne Kaskazini mwa Nigeria.
Kamishna wa polisi Lawan Tanko amethibitisha mashambulizi hayo ingawa hakutoa maelezo zaidi.
Eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, limekuwa chini ya sheria ya hali ya hatari tangu mwezi Mei mwaka jana
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni