Na Eleuteri Mangi-Maelezo Mtwara
SERIKALI imewapa jukumu wananchi wanaoishi maeneo linapopita  bomba la kusafirishia gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam la kulitunza na kulilinda  kwa manufaa yao na taifa zima.
Wito huo ulitolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda  leo alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa bomba hilo.
Waziri Mkuu Pinda alisema Serikali inavihakikishia vijiji lilipopita bomba hilo kuwa watapatiwa umeme unaotokana na uzalishaji wa gasi na utakuwa wa gharama nafuu.
Zaidi ya hayo, gasi itatumika kwa matumizi ya nyumbani kwa kuunganishiwa bomba la gasi na ambao hawatafanikiwa watakuwa na fursa ya kupata mitungi ya gesi ambayo itakuwa ya bei nafuu.
Waziri Mkuu ameagiza mashirika ya Shirika la gasi na Petroli Tanzania (TPDC) na Mradi wa Nishati Vijijini (REA) wachukue jukumu la kuboresha maisha ya wananchi wa maeneo lilipopita bomba hilo katika maeneo ya barabara, shule, kuwapatia maji safi na salama,kuwaboreshea utoaji wa huduma za afya kwa kuboresha zahanati na vituo vya afya kama mchango wao kwa jamii.
Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alisema kuwa serikali kupitia shirika la TPDC na REA itahakikisha wanachi waishio vjijini wanapata umeme mapema iwezekanavyo.
Kwa kuthibitisha kauli hiyo Prof. Muhongo alisema serikali kupitia TPDC na REA imetenga sh. Bilioni 20 kwa awamu ya kwanza ambayo itasimamiwa na REA wakati awamu ya pili nayo itatumia bilioni 20 iotkaysimamiwa na TPDC.
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu aliambatana na mke wake bi Tunu Pinda, Balozi wa China nchini, Lu Younqing, Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, mbunge wa Mchinga Said Matanda na Fatma Mikidadi mbunge wa viti maalum.
Maeneo aliyotembelea Waziri Mkuu ni pamoja na Vikindu, Jopika, Bungu, Ikwiriri, Somanga, Somanga Fungu, Kitomanga na Lindi.
(Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO-Mtwara) Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akieleza hatua iliyofikiwa katika ujennzi wa bomba la gasi linalojengwa kutoka Mtwara hadi Dar es salaam kwa Waziri Mkuu na msafara wake. Kushoto ni Balozi wa China nchini, Lu Younqing.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akieleza hatua iliyofikiwa katika ujennzi wa bomba la gasi linalojengwa kutoka Mtwara hadi Dar es salaam kwa Waziri Mkuu na msafara wake. Kushoto ni Balozi wa China nchini, Lu Younqing.
……………………………………………………………………………………..
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni