Watu wawili ambao hawajafahamika majina yao wameuwawa kwa kuchomwa moto na wananchi wanaozaniwa kuwa na hasira kali katika kijiji cha Kagongwa wilayani Kahama Mkoani Shinyanga baada ya kudaiwa kuiba vitu mbalimbali ikiwemo Komputa.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa tano asubuhi baada ya watuhumiwa hao kujaribu kuwakimbia viongozi wa Sungusungu waliokuwa wanawashikilia baada ya kuwakamata.
Kwa mujibu wa Mashuhuda wamesema vijana hao walikuwa ni tishio katika mji huo kutokana na kutuhumiwa kufanya vitendo wa wizi mara kwa mara.
Wananchi wenye hasira kali baada ya kuwakamata wameamua kuwachoma moto kwa madai kuwa iwe ni fundisho kwa wengine.
Wamesema Awali watuhumiwa walikamatwa na sungusungu ya kijiji cha Iponya wilayani humo kabla ya kuamriwa wakaoneshe vitu hivyo ndipo wakapata mwanya wa kukimbia.
Diwani wa kata ya Kagongwa Hamis Kashantole ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa kata hiyo amekataa kuzungumzia tukio hilo kwa madai kwamba hana muda wa kuongea.
Jeshi la polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi unaendelea
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni