Mtendaji wa kijiji cha Kalenga akimkaribisha Kiswaga kuzindua kikundi hicho |
MKURUGENZi wa kampuni ya simu ya Tigo kanda ya nyanda za juu kusini Jackson Kiswaga amechangia kiasi cha Tsh 700,000 kwa ajili ya kukiwezesha kiuchumi kikundi cha Vicoba cha Twiyendage kata ya Kalenga wilaya ya Iringa .
Kiswaga alikabidhi msaada huo leo wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho chenye wanachama 30 kama njia ya kuunga mkono jitihada za wanawake hao katika kujiletea maendeleo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho Kiswaga aliwataka wanachama wa kikundi hicho kuzidi kuwahamasisha wenzao kujiunga na vikundi kama hivyo kama njia ya kujikwamua kiuchumia na kuwataka wanachama kujenga utamaduni wa kurejesha mikopo pindi wanapokopeshana .
Kwani alisema iwapo wanachama wengi zaidi watahamasishwa kujiunga na vikundi hivyo vya kiuchumia upo uwezekano mkubwa wa serikali na taasisi mbali mbali za kifedha kuunga mkono jitihada za vikundi hivyo.
"Awali ya yote ninapenda kuwashukuru wanachama kwa kunialika kuwa mgeni rasmi hapa leo ila bado napenda kuwatia nguvu kwa kuwachangia kiasi cha Tsh 700,000 ili kuongeza mtaji wenu zaidi ... ili kuweza kujikomboa kimaisha ni lazima kuanzisha vikundi kama hivi vya kiuchumia"
Awali mwenyekiti wa kikundi hicho Mwahija Witala alisema kuwa kikundi hicho kina wanachama 30 kutoka makundi mbali mbali ya kijamii wakiwemo walimu, wakulima wafanyabiashara na wa wale wasio kuwa na ajira .
Witala alisema hadi sasa kikundi hicho kina mtaji wa Tsh milioni 3 na lengo ni kuendelea kusaidiana zaidi ikiwa ni pamoja na kusaidia makundi mbali mbali ya jamii yaayowanzunguka wakiwemo watoto yatima.
Kiswaga akiwa na wanachama wa kikundi cha Vicoba Twiyendage Kalenga mara baada ya kuzindua kikundi hicho |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni