Kilosa, Morogoro
Makamu wa Rais Mhe Mohamed Gharib Billali pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (MB)Jumamosi tarehe 29/3/2013 walishiriki mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe John Gabriel Tuppa ambaye alifariki ghafla wiki iliyopita.
Katika Mazishi hayo yaliyofanyika Kilosa mjini Mkoani Morogoro yalihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mheshimiwa Steven Wassira, Waziri wa Ardhi Prof Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Hawa Ghasia. Aidha Manaibu Waziri kadhaa walikuwepo akiwepo Mhe Aggrey Mwanri (MB), Naibu Waziri wa OWM TAMISEMI, Mhe Kebwe Stephen Kebwe (MB) Naibu Waziri wa Afya. Wakuu wa Mikoa nao walishiriki mazishi ya mwenzao.
Aidha Wakuu wa Wilaya kadhaa nao walishiriki wakiwemo Wakuu wa Wilaya za Mikoa ya Mara na Morogoro na Wakurugenzi wao.
Makamu wa Rais akitoa heshima za mwisho
Makamu wa Rais akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Tuppa
Makamu wa Rais akiweka shada la Maua
Makamu wa Rais akimfariji mke wa Marehemu Tuppa
Makamu wa Raisi akimfariji baba mzazi wa Marehemu Mzee Gabriel Tuppa
Makamu wa Raisi akimfariji baba mzazi wa Marehemu Mzee Gabriel Tuppa
Pichani Waziri Mkuu akiweka udongo katoka kaburi la marehemu Tuppa
Mhe Pinda akimfariji Mzee Gabriel Tuppa ambaye ni baba mzazi wa Marehemu John Tuppa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni