Watu 15 wameaga dunia katika msongamano uwanjani Kinshasa
Ghasia.
Ghasia zilizozuka baada ya mechi ya soka timu mbili maarufu za Klabu ya ASV
na Tout Puissant Mazembe zilipokuwa zikichuana katika mechi ambayo ingeamua
muakilishi wa DRC katika kombe la bara Afrika mwakani.
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema ghasia hizo zilianza dakika za mwisho
za mechi baada ya timu ya Tout Puissant Mazembe kuongoza kwa bao moja na
mashabiki wakaanza kurusha mawe uwanjani na kujeruhi baadhi ya wachezaji.
Refa alilazimika kusimamisha mechi hiyo.
Polisi walirusha gesi ya kutoa machozi ili kutawanya mashabiki waliokuwa
wakipambana na kusababisha watu kuanza kukimbia na kukanyagana.
Gavana wa mji wa Kishasa amesema serikali itachunguza tukio hilo na
waliohusika watachukuliwa hatua kali (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni