Jumatatu, 30 Juni 2014

MAMA ALIYEUA 'MWANAYE' KIZIMBANI

Amina Ibrahim (27), mkazi wa Kimara jijini Dar anayeshikiliwa kwa kesi ya kumuua 'mwanaye'.
MKAZI wa Kimara Amina Ibrahim (27), amepandishwa Kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka la kumuua mtoto wake wa kambo.
Akisomewa kosa hilo leo mbele ya Hakimu Amalia Mushi, Wakili wa Serikali Faustine Sylivester, alidai kuwa tukio hilo lilitokea Juni 18 mwaka huu huko Kimara, Wilaya ya Kinondoni.

Sylivester alidai kuwa mshitakiwa alikuwa akiishi naye na ndipo alipoamua kumuua mtoto huyo ajulikanaye kwa jina la Munir Dodi (6), wakati akifahamu kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu kitu chochote kutokana na kosa lake kwani Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, hivyo kesi imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni