Alhamisi, 26 Juni 2014

MIKOSI YAMWANDAMA MWAMKE ALIYEASI DINI HUKO SUDAN


Mwanamke aliyeasi dini 'ameghushi' hati
Mwanamke wa Sudan aliyeachiwa huru baada ya kuhukumiwa kifo kwa madai ya kuasi anatuhumiwa kughushi hati.
 
Mwanasheria wa mwanamke wa Sudan aliyekamatwa siku chache baada ya kuachiwa baada ya kuhukumiwa kifo kwa kuasi dini ya Kiislam kwa kuolewa na Mkristo, amesema mteja wake anatuhumiwa kwa kughushi nyaraka za safari.
Amesema mwanamke huyo Meriam Ibrahim bado anashikiliwa katika kituo cha polisi katika mji Mkuu wa Khartoum.
 
Sudan Kusini ambayo ndio iliyompa nyaraka hizo imesema kuwa nyaraka hizo ni halali kwa vile ameolewa na mwanaume raia halisi wa Sudan Kusini.
Mwanasheria wa Meriam Ibrahim amesema yeye pamoja na mumewe walikuwa wakiohojiwa kuhusuana na hati za kusafiria. Ilikuwa inasadikiwa kuwa walikuwa wanasafiri kuelekea nchini Marekani.

Meriam Ibrahim na mumewe
Awali Marekani ilisema itashirikana na Sudan kuhakikisha kuwa mwanamke aliyesamehewa hukumu ya kifo kwa kuasi dini ya Kiislam anaruhusiwa kuondoka nchini humo baada ya kukamatwa katika uwanja wa ndege wa Khartoum.
Mwanamke huyo Meriam Ibrahim, alihukumiwa kifo kwa kosa la kuolewa na mwanamume mkristo na kukana dini ya kiisilamu alikamatwa akiwa na familia yake katika uwanja wa ndege mjini Khartoum.
Watu waliomkamata walikuwa wamevalia mavazi ya kiraia ingawa wanaaminika kuwa wanajeshi wa serikali.
Duru zinasema kuwa Meriam Ibrahim aliyejifungulia jela alikuwa anajiandaa kuondoka nchini Sudan pamoja na familia yake.
Haijulikani kwa nini alikamatwa na karibu watu arobaini waliokuwa wamavalia mavazi ya kiraia siku moja tu baada ya kuachiliwa huru kutoka jela ambapo mahakama ya rufaa ilibatilisha hukumu yake ya kifo.

Meriam na muwewe siku ya harusi
Meriam alikamatwa kwa mara ya kwanza mwezi Februari na baadaye kujifungua mtoto wake msichana jela baada ya kuhukumiwa kifo.

Familia yake imepelekwa katika makao makuu ya idara ya ujasusi.
Kabla ya kuzuiliwa kwake tena, jamii ya kimataifa ilipongeza uamuzi wa kuachiliwa kwake na kumuondolea hukumu ya kifo chake BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni