Polisi nchini kenya wamemtia mbaroni gavana wa jimbo la Lamu
lililokumbwa na mapigano hivi majuzi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya
65.
Polisi walimshika Issa Timamy kufuatia tuhuma za kuhusika na mashambulizi
yaliyotokea Mpeketoni mapema mwezi huu.Punde baada ya tukio hilo rais Uhuru Kenyatta alikatalia mbali madai kuwa ilikuwa shambulizi la kigaidi lililotekelezwa na kundi la waislamu la Al Shaabab.
Kundi la wapiganaji kutoka Somalia Al Shabab lilidai kutekeleza shambulizi hilo.
Bwana Timamy ni Gavana wa pekee kutoka chama cha UDF .
Aidha wavamizi waliwalenga wanaume ambao hawakuwa waislamu na kuwataka kukariri shahada ama aya za Quran, wale walioshindwa waliuawa .
Siku ya jumatano maafisa wa utawala katika jimbo hilo la Lamu walidai kuwa wamewakamata watu 13 waliokuwa wakipanga njama ya kufanya uvamizi zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni