Ijumaa, 27 Juni 2014

MWANAMKE AJIFUNGUA MTOTO BAADA YA KUBEBA MIMBA KWA MIAKA 14


'Mwanamke wa Nigeria aliyejitambulisha kwa jina la Mercy James amesimulia tukio la ajabu la kujifungua salama mtoto wa kike baada ya kuwa mjamzito kwa kipindi cha miaka 14. Mtoto aliyeamua kumuita ‘Miracle’

Kwa mujibu wa Vanguard, Mercy alieleza kuwa alianza kujisikia dalili za ujauzito miaka 14 iliyopita lakini awali dalili hizo zilikuwa zinabadilika na mara nyingine anaingia katika hedhi kwa siku moja, lakini hali ilianza kuwa serious miaka miwili baadae alipoenda hospitali na kuhakikishiwa kwa vipimo kuwa ni mjamzito. Nilienda tena kwa tabibu miaka miwili baadae na kumlalamikia kuhusu maumivu niliyokuwa nayapata, aliniambia tena kuwa sina tatizo la tumbo na kwamba huo ulikuwa ujauzito. Alinishauri niendelee na maombi ili Mungu aniepushe na mikono ya shetani.
Mercy alisimulia.
Anaeleza kuwa alikuwa anatumia madawa mengi ya kutibu magonjwa ya tumbo lakini hali yake haikubadilika.
Hali iliendelea hivyo hadi ilipofika June 7 mwaka huu ambapo alienda tena katika hospitali hiyo akiwa analalamika na kusikia kila dalili za kitu kutaka kutoka mwilini mwake, lakini hakufahamu kuwa hiyo ingekuwa siku ambayo angejifungua mwanae wa kike, ‘Miracle’.
Kisha Mungu aliamua kunifuta machozi. Katika siku niliyojifungua mwanangu wa kike, mwanzo nilihisi ni minyoo inataka kutoka kwenye mwili wangu bila kufahamu kuwa yule alikuwa mtoto. Hivi ndivyo nilivyomwambia mkunga. Lakini baada ya kunipima alianza kuniambia nisukume. Nilimpotezea. Baadae nikaishiwa fahamu kama dakika 15 na nilipopata fahamu, nilisikia mtoto Analia. Nilishangaa sana na kuchanganyikiwa nilipomuona mwanangu. Sikuweza kuamini macho yangu.
Mercy aliendelea kusimulia tukio hilo.
Naye tabibu wa hospitali ya kanisa la ‘Celestial Church Of Christ, Parokia ya Kadoso ambapo Mercy alijifungulia, aliyetajwa kwa jina la Ajegunle aliliambia Vanguard kuhusu hatua zote alizopitia hadi kujifungua mwanae huyo na jinsi yeye binafsi kama mkunga alivyohusika.
Marafiki na ndugu wa mwanamke huyo walitoa ushuhuda pia kwa gazeti la Vanguard la Nigeria kuhusu tukio hilo la kushangaza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni