Jumatatu, 2 Juni 2014

WANAHARAKATI MJINI KISUMU WALALAMIKIA KUONGEZEKA VITENDO VYA UBAKAJI

Activists protest rising rate of <a href='http://www.standardmedia.co.ke/thecounties/search?q=rape'> rape</a> in Kisumu
Kamanda wa Polisi Kisumu  David Ngetich.

Kisumu, Kenya: Watetezi wa haki za watoto mjini Kisumu wamelalamikia kuongezeka kwa vitendo vya ubakaji katika eneo la Kisumu.

Zaidi ya kesi 60 za ubakaji na unajisi wa watoto zimeripotiwa mwaka huu pekee, jambo ambalo wanaharakati wanadi kuwa ni kutokana na uzembe ndani ya jeshi la Polisi.

Helen Apiyo, kiongozi wa shirika la Watoto Msilie, anasema kuwa washukiwa hupotea baada ya kupata dhamana mahakamani.

‘‘Polisi wanatakiwa kuhakikisha kuwa watuhumiwa hawa wa vitendo hivi viovu wanasakwa na kufikishwa mahakamanina pia Polisi wanatakiwa kupewa mafunzo maalumu ili kuweza kufuatilia kesi za unajisi wa watoto..’’ alisema Apiyo.

Katika maeneo ya makazi yasiyo rasmi kama Nyalenda wabakaji wanawadanganya watoto wadogo kuwa pipi na baadaye kuwafanyia unyama huo>

Miezi miwili iliyopita mwanamume mwenye umri wa kati anatuhumiwa kumnajisi mtoto wa miaka 9 katika shule moja mjini hapa. Pia aliwarubuni watoto wengine wawili wa shule walipokuwa wanacheza kwa pipi ni kuwanajisi kwa nyakati tatu tofauti.(TK)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni