Jumatatu, 2 Juni 2014

BOKO HARAM YAWAACHIA MAKASISI WAWILI WALIOWATEKA


Kituo cha uhamiaji kati ya mpaka wa Cameroon na Nigeria
 

Makasisi wawili kutoka nchini Italy pamoja na mwanamke mmoja raia wa Canada waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram nchini Cameroon wameachiliwa huru.

Idara ya mawasiliano nchini Cameroon imesema watatu hao wako katika afya nzuri na wamesubiri ndege inayoelekea katika mji mkuu wa Younde.

Walipelekwa kaskazini mwa taifa hilo karibu na mpaka na Nigeria.

Majina ya makasisi hao ni Giampaolo Martana na Giantonio Allegri (TK).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni