Boko Haram wamekuwa wakifanya mashambilizi ya mara kwa mara
licha ya operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji hao
Takriban watu watano wameripotiwa kuuawa katika mlipuko
uliotokea sokoni Maiduguri kaskazini mwa Nigeria.
Watu walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kuwa gari lililokuwa limebeba
mkaa lilipuliwa na bomu linalodhaniwa liliwekwa ndani ya gari hilo.
Hadi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililokiri kuandaa shambulio
hilo.
Tukio hili linakuja huku ripoti ya hivi karibuni ya jeshi la Nigeria ikisema
kuwa limeshambulia moja ya ngome za kundi la wapiganaji la Boko Haram.
Mwandishi wa BBC Habiba Adamu toka mji mkuu wa Nigeria Abuja aliyetembeela
eneo hilo anasema kuna utata wa idadi ya waliouawa katika shambulio hilo kwani
wakati wengine walisema waliouawa ni watano wengine wanasema huenda idadi ya
waliouawa ikawa ni zaidi ya hiyo iliyotolewa(TK).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni