Jumanne, 15 Julai 2014

POLISI MJINI MOMBASA WAKAMATA 'UNGA' WA MABILIONI

NAIROBI, KENYA: Maafisa usalama mjini Mombasa wamekamata kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya aina ya heroine.


Afisa anayeshughulikia madawa ya kulevya Hamis Masha amesema kuwa mzigo huo ulikuwa na kilo  341.7 na thamani yake ni Sh za Kenya 1.1 billion kwenye meli ya MV Bushehr Amin Darya ambayo ilikuwa imesimama majini.

Wiki iliyopita polisi walikamata watu wawili wakiwa na kilo moja ya dawa za kulevya.

Pwani ya  Kenyan imekuwa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni baada ya  Uongoziwa Australia kukamata kiasi kikubwa cha dawa za kulevya. (TK)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni