Jumanne, 15 Julai 2014

WATU 50 WAUAWA KATIKA SHAMBILIZI AFGHANISTAN


Takriban watu 50, wameuawa katika shambulizi la bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari katika soko moja lenye shughuli nyingi , katika mkoa wa Paktika, Mashariki mwa Afghanstan.
Soko lilikuwa na idadi kubwa ya watu wakati wa shambulizi lilipofanyika.
 
Maafisa wa usalama wanasema kuwa mshukiwa mmoja aliyekuwa ameandamwa na polisi alitegua bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari lake katika eneo lililokuwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wananunua vitu kutumia wakati huu wa Ramadhan.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa mkoa wa Paktika ni ngome ya wapiganaji wa mtandao wa Haqqani na hushuhudia mashambulizi ya mara kwa mara.
Hakuna kundi lililokiri kufanya shambulizi hilo.
Awali polisi walisema kuwa wanaume wawili waliokuwa wakimfanyia kazi Rais anayeodnoka mamlakani Hamid Karzai wameuawa katika shambulizi lengine la bomu mjini Kabul.
Bomu hilo linalokisiwa kutegwa kando ya barabara lililipuka karibu na gari ambalo wawili hao walikuwa wakisafiria kwenda kazini .
Kundi la Taliban limekiri kuhusika na shambulizi hilo ambalo pia liliwajeruhi watu wengine watano.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni