Makamu wa Rais wa Marekani John Kerry akiongoza mazungumzo moja ya vikao kati ya Israel na Palestina ili kumaliza vita (picha na Maktaba).
Mazungumzo ya Amani kati ya Israel na Palestina
Wajumbe wanaowakilisha Israel na Palestina wanakutana katika mji mkuu wa Cairo nchini Misri siku ya jumapili ili kuendelea na mazungumzo yao yasio ya moja kwa moja kutafuta mwafaka wa kusitisha vita katika eneo la Gaza
Pande zote mbili zinatekeleza makubaliano ya siku tano ya kusitisha vita yanayokamilika siku ya jumatatu usiku.
Siku ya Alhamisi wakati mazungumzo yalipokwisha wawakilishi wa Palestina walisema kuwa wanachukua tahadhari kuhusu maendeleo ya mazunngumzo hayo.
Kundi la wapiganaji wa Hamas linataka Israel na Misri kuondoa vikwazo vya mipakani dhidi ya Gaza huku Israel ikilitaka kundi la Hamas kusalimisha silaha zao na kuacha kurusha makombora nchini Israel.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni