Mhe Rais Dkt Jakay Kikwete ameanza ziara rasmi ya kuutembelea mkoa wa Morogoro.
Ziara hiyo ilianzia Mwaya Wilayani Ulanga ambapo tarehe 20 Agosti alifungua mradi wa umeme wa REA eneo hilo. Aidha alikagua mpango wa Telemedicine katika kituo cha afya Mwaya. Telemedicine ni mpango unaounganisha kituo cha afya na madaktari bingwa nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni