Ismail Gunduz akimpiga kichwa refa naye refa (mwnye T shirt ya njano) anaonekana akianguka
Mchezaji Ismail Gunduz wa SK Rum ya Austria amefungiwa kuto
cheza mechi 70 ikiwa ni adhabu baada ya mchezaji huyo kumpiga kichwa uwanjani
mwamuzi wa mchezo.
Gunduz anayechezea timu ya daraja la tano ya SK RUM alimpiga mwamuzi siku ya
Jumamosi kwa kichwa muda mfupi kabla ya mwamuzi huyo kupuliza kipenga cha
kumaliza mchezo.
Hata hivyo mwamuzi huyo alikimbizwa hospitali kwa matibabu kutokana na
maumivu aliyoyapata baada ya kupigwa kichwa hicho.
Kwa mjibu wa sheria za soka za taifa hilo adhabu ya juu kwa kosa kama hilo ni
kufungiwa michezo 108
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni