Jumapili, 7 Juni 2015

MAKONGORO NYERERE AMRUSHIA MADONGO WASSIRA

https://sundayshomari.files.wordpress.com/2015/06/makongoro.jpg?w=714

"Tangu nikiwa kijana mdogo nasoma sekondari, wakati huo Mwalimu Nyerere akiwa Rais wa nchi hii, Mzee Steven Wassira amekuwepo kama Kiongozi. 



Huyu ni mtu ambaye amekuwa Kiongozi katika awamu zote za uongozi, haingii akilini anaposema nikiingia Ikulu jembe la mkono litakuwa historia.


"Sina shaka kabisa kuhusu uadilifu wake lakini kwa nafasi alizoshika miaka yote hii alitakiwa aseme jitihada alizofanya kufanya jembe la mkono kuwa historia.

"Hata hivyo ingefaa sana endapo viongozi wetu wangeanza kuheshimu utamaduni wa kung'atuka ili kutoa nafasi kwa watanzania wengine kulitumikia Taifa."

  Alisema Makongoro Nyerere alipokuwa anatangaza nia yake ya kuteuliwa na CCM ili kugombea Urais)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni