Alhamisi, 4 Septemba 2014

DIAMOND AFUNGUKA: NILIDHALILISHWA UJERUMANI


Stori: Shakoor Jongo
SIKU chache baada ya kufanyiwa fujo katika shoo yake nchini Ujerumani, staa wa Mdogo Mdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibuka na kueleza namna ambavyo alidhalilishwa nchini humo.
Diamond aliponea chupuchupu kupewa kipigo baada ya kuchelewa kwenye shoo iliyokuwa ifanyike katika Ukumbi wa Sindelfingen katika mji wa Stuttgart, Ujerumani.

Staa wa Mdogo Mdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akizungumza na paparazi wetu baada ya kutua Bongo Jumanne iliyopita, Diamond alisema anasikitika kwani alidhalilishwa wakati alipokuwa akidai haki ya kumaliziwa malipo yake ya shoo euro 250 (zaidi ya sh 500,000).GPL(P.T)
“Inaniuma sana kwani mimi pale nilikuwa nasimamia haki yangu, kwani nilikuwa nawadai euro 250 sasa nikaona wananizungusha na nilipokomaa zaidi huku wakiona muda wa shoo unapita, ndipo walipoanza kunitukana bila sababu.
“Wamenitukana mimi, wamewatukana hadi ndugu zangu ambao hawakuhusika na chochote na wala hawakuwepo kule. Wamenidhalilisha bila kosa. Kimsingi sikutaka kupanda jukwaani pasipo kumaliziwa fedha zangu licha ya kuwa si nyingi kiivyo,” alisema mtoto huyo wa Tandale.

Hali halisi ya ukumbi nchini Ujerumani ulivyoharibiwa na mashabiki waliovurugwa kwa kucheleweshewa shoo ya Diamond.
 
Kwenye maelezo mengine na paparazi wetu, Diamond alisema baada ya kutokea vurugu hizo alilazimika kurejea nchini pasipo kumaliziwa fedha zake lakini promota wa shoo hiyo, Kamabritts aliahidi kuandaa shoo nyingine ya bure ili kujisahihisha kwani kosa lilikuwa la kwake.
 
Kwenye mvutano huo kati ya msanii na promota huyo, Diamond alitegemewa kupanda jukwaani saa nne usiku lakini ilishindikana hadi ilipofika saa 10 alfajiri kitendo ambacho kilisababisha mashabiki wafanye vurugu kwa kuvunja viti na thamani nyingine za ukumbi zinazokadiriwa kufikia Euro 128,222 (Sh. milioni 280).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni