Rais wa
jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipunga
mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa
Uhuru, Jijini Dar es salaam, leo kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za
Maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto
ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange .Picha na OMR
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua
gwaride la heshima, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru,
jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wa Serikali, wakisimama kutoa
heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo. Picha na OMR
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni