Rais
wa Burundi, Pierre Nkurunziza akirejea nchini mwake baada kushindikana
kwa jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali yake alipokuwa nchini
Tanzania kuhudhuria kikao cha viongozi wa EAC.
Rais wa
Burundi, Pierre Nkurunziza amejerea nyumbani hapo jana, baada ya kuwepo
kwa jaribio la kumpindua akiwa nchini Tanzania kuhudhuria kikao cha
viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokuwa wakijadili mgogoro wa
Burundi.
Maafisa wa serikali wanasema kurejea nyumbani kwa Rais huyo sasa ni ishara kuwa jaribio la kumpindua limeshindikana.
Wakati
huo huo Mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Jenerali Niyongabo amesema vikosi vya
serikali ya Burundi vimefanikiwa kudhibiti hali ya mambo na kuzima
jaribio la kumpindua Rais Pierre Nkurunziza.
Tayari
vikosi vya serikali vimewatia nguvuni baadhi ya wanajeshi waliokuwa
wakijaribu kuipindua serikali huku baadhi yao wakijitetea kuwa
walirubuniwa.
Hapo jana
kulikuwa na mapigano makali karibu na radio ya taifa kati ya majeshi
yaliyojaribu kuipindua serikali na yale yanayomtii Rais Pierre
Nkuruziza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni