RAis
mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin Mkapa akifungua Mkutano wa mwaka
wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi leo jijini Dar es salaam.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia masuala mbalimbali. Picha/Aron Msigwa -MAELEZO.
Na Aron Msigwa,MAELEZO .
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin Mkapa amewataka Wakandarasi kote
nchini kufanya kazi zao kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni na
taratibu zinazosimamia Sekta ujenzi ili miradi wanayoisimamia na
kuitekeleza iweze kuwa na manufaa kwa taifa.
Mhe.Mkapa
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano
wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) uliowawajumuisha pia
wadau wa sekta ya Ujenzi kutoka nchini Malawi na Kenya.
Amesema
umakini katika usimamizi wa kazi za wakandarasi na uwepo wa wataalam
waliobobea katika sekta ya ujenzi umechangia kwa kiasi kikubwa kasi
maendeleo inayotokea sasa nchini Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni