Alhamisi, 14 Mei 2015

WAASI WA UG WAUA WATU 23 DRC


Waasi DRC

Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema kuwa watu ishirini na watatu wameuawa kikatili na wapiganaji wa UG wanaodaiwa kuwa waasi wa Uganda.
Wanane kati ya waliofariki ni wanajeshi wa DRC.
Shambulizi hilo lilifanyika Jumatano usiku.
Waasi wengi wao wakiwa wa Allied Democratic Forces (ADF) wamefanya mashambulizi kadhaa kusini mwa mji wa Beni katika siku za hivi karibuni.
Umoja wa mataifa unasema kuwa huenda walifanya makosa ya uhalifu wa kivita na vitendo vinavyokiuka ubinadamu.
ADF imewaua mamia ya watu wakati mwingine na nondo, panga na visu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni