Alhamisi, 14 Mei 2015

MAKUNDI HASIMU YAPAMBANA BUJUMBURA

 
Wanajeshi Burundi
Makundi hasimu ya askari yanakabiliana katikati mwa mji mkuu wa Burundi- Bujumbura, mahala ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza, amepinduliwa.
Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika.
Radio na Luninga ya taifa inang'ang'aniwa kwa sasa huku wanajeshi waaminifu kwa rais Nkurunziza ndio wanaoidhibiti.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni