Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 48 ambaye anafundisha katika shule moja katika
Rachuonyo North Sub County. Inadaiwa kuwa mwalimu h umri wuyo alimuoa mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 17kama mke wake wa tatu.
Mwalimu huyo alimuoa mwanafunzi huyo ambaye alikuwa amepanga nyumba moja katika Othiere Trading Centre kuanzia mwezi July.
Kulingana na baba mzazi wa mwanafunzi huyo mwalimu huyo ambaye alimfundisha mwanaye shule ya msingi anasadikiwakuanza mahusiano na mwanafunzi huyokabla hajaanza shule ya upili,
"Kuna siku nilimkamata mwalimu huyo na binti yangu lakini mwalimu huyo akatimua mbio.
Mmoja wa wake zake alikuja nyubani na kumtishia mwanangu kuwa ana mahusiano na mume wake," alisema baba huyo.
Hata hivyo, Mkuu wa Polisi wa Rachuonyo Kusini OCPD Patricia Nasio alisema kuwa mwalimu huyo alikanusha madai hayo na kujitetea kuwa alikuwa akiishi na binti huyo baada kwenda kuomba hifadhi. Alidai kuwa baba wa msichana huyo alikuwa amemfukuza kutokana na kudai kuwa hana nidhamu.
Mwalimu huyo alisisitiza kuwa alikuwa anasubiri hasira ya baba yake ipoe ndipo amrudishe nyumbani. Maelezo ya Mwalimu huyo yaliungwa mkono na binti huyo
Baba mzazi wa dent huyo alikanusha madai ya mwalimu huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni