Baada ya kuitandika Basle 5-0 katika Champions League, kisha wakaja kuifumua Deportivo La Coruna 8 kwenye La Liga wikiendi iliyopita, jana kipigo cha Madrid kilihamia kwa timu ya Elche katika La Liga. Wakicheza kwenye dimba lao la Santiago Bernabeu Madrid walianza kwa kuanza kufungwa goli na Elche kupitia mchezaji Gallego, lakini dakika chache baadae Gareth Bale akasawazishia Madrid. Cristiano akafungua akaunti yake ya magoli jana kwa kufunga penati katika dakika ya 28, dakika baadae akaongeza kwa kichwa, kisha akafunga la penati tena dakika 80 kabla ya kumalizia shughuli kwa la tano dakika ya tisini ya mchezo.
Ronaldo akaweka rekodi ya kufunga hat trick ya 25 tangu alipojiunga na Real Madrid mwaka 2009 – huku akiisaidia Madrid kutimiza magoli 18 ya kufunga katika mechi 3 zilizopita.
Timu zilipangwa kama ifuatavyo:
Real Madrid: Navas, Marcelo, Carvajal, Varane, Ramos, Kroos, Rodríguez, Illarramendi, Bale, Isco, Ronaldo
Subs: Casillas, Coentrão, Benzema, Hernández, Arbeloa, Nacho, Modric
Booked: Carvajal, Marcelo
Scorers: Bale 20′, Ronaldo 28′, 32′, 80′, 90′
Elche: Yagüe, Gallego, Pelegrín, Lombán, Cisma, Romero, Corominas, Rodrigues, Mosquera, Morales, Cristian de Jesus
Booked: Gallego
Scorer: Gallego 15′
Subs: Suárez, Roco, Herrera, Martín, Fajr, Pasalic, Tyton
Ref: Carlos Clos Gómez
At: 65,000
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni