Watu watano wamehukumiwa kifungo cha miaka 37 jela na kuchapwa viboko 24 kila mmoja
baada ya kupatikana na hatia ya kuvamia na kupora fedha benki ya NMB tawi la
Maswa kwa kutumia silaha.
Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga na kusikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo,
Neema Gasabile ambapo alitoa hukumu hiyo.
Aliwahukumu kifungo cha miaka
37 na viboko 24 kila mmoja viboko 12 wakati wa kuingia na 12 wakati wa kutoka
baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashitaka kuwa kwa
pamoja walitenda kosa hilo kinyume cha sheria.
Washitakiwa hao ni Kapama
Hamis Ramadhan (37), Mussa Athuman Buberwa (38), Amos Mathayo, Lucas Vincent
Mabela (40) na Zainabu Mchau (60) wote kwa pamoja walipatikana na hatia ya
makosa tisa ya jinai.
Mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Mwendesha
Mashitaka Mwanasheria wa Serikali Edith Tuka aliieleza mahakama hiyo kuwa
washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo majira ya saa 6:00 mchana Julai
5, mwaka 2010 mjini Maswa.HABARILEO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni