Mshambuliaji Danny Welbeck akishangilia baada ya kupiga 'hat-trick'.
Alexis Sanchez akiifungia Arsenal bao la tatu dhidi ya Galatasaray.
Welbeck akitupia bao la nne.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametimiza miaka 18 akiwa meneja wa klabu hiyo leo.
KLABU ya Arsenal imetoa kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Galatasaray kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopigwa Uwanja wa Emirates jijini London usiku huu.
Mshambuliaji Danny Welbeck ametupia kambani mabao matatu 'hat-trick' huku bao la nne likiwekwa kimianai na Alexis Sanchez. Katika mtanange huo, kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny alizawadiwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Galatasaray, Burak Yilmaz.
Ushindi wa leo wa Arsenal umeongeza furaha kwa Meneja wa timu hiyo, Arsene Wenger aliyetimiza miaka 18 akiwa kocha wa klabu hiyo leo.
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Cazorla, Ozil (Wilshere 77), Sanchez (Ospina 62), Oxlade-Chamberlain (Rosicky 68), Welbeck.
Waliokuwa benchi: Coquelin, Bellerin, Campbell, Podolski.

Galatasaray: Muslera, Chedjou, Felipe Melo, Semih Kaya, Veysel (Bulut 68), Yekta (Altintop 46), Dzemaili, Telles, Sneijder, Pandev (Bruma 68), Burak Yılmaz.
Waliokuwa benchi: Bolat, Balta, Adin, Camdal.
Waliokuwa benchi: Bolat, Balta, Adin, Camdal.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni